Na Shomari Binda-Musoma
WADAU wa elimu na wazawa wa Kata ya Nyakatende jimbo la Musoma vijijini wameombwa kujitokeza kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa shule shikizi ya Kiunda.
Harambee biyo itafanyika januari 12 kwenye Kitongoji cha Kiunda Kijiji cha Kamguruki Kata ya Nyakatende kuanzia SAA 8 mchana.
Shule shikizi ya Kiunda inajengwa kwenye Kitongoji hicho ili kuweza kuwasaidia watoto wa elimu ya awali kusoma jirani na maeneo wanayoishi.
Watoto wa vitongoji 3 watasoma na kuandaliwa kwenye shule hiyo na baadae kwenda kwenye shule za msingi kwenye maeneo mengine.
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini atakayeongoza harambee hiyo amewaomba wadau na wazawa wa Kata ya Nyakatende kujitokeza kwenye harambee hiyo.
Amesema maandalizi ya kupokea elimu yanatakiwa kuandaliwa toka awali na watoto wanapaswa kusoma jirani na nyumbani.
Muhongo amesema kukamilika kwa shule hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa watoto kuweza kusoma jirani na nyumbani.
“Elimu inaanzia ngazi ya awali hivyo ni muhimu kuwawekea mazingira mazuri watoto wetu kupata elimu hivyo nawaomba tujitokeze kwenye harambee“,amesema.
Aidha kwa wale wasiopata nafasi ya kufika kwenye harambee wawasilishe michango kwenye akaunti ya benki ya NMB namba 30302300679
kwa jina la Kijiji cha Kamguruki