Home Biashara WADAU WA MAONYESHO YA BIASHARA SABASABA 47 WAJIPANGA KIPEKEE; KARIBU USISUBIRIE KUSIMULIWA

WADAU WA MAONYESHO YA BIASHARA SABASABA 47 WAJIPANGA KIPEKEE; KARIBU USISUBIRIE KUSIMULIWA

Na Magrethy Katengu

Wadau wa Maonyesho ya biashara wamesema mwaka huu katika sabasaba itakiwa ya kipekee hivyo kutakuwa na fursa nyingi Tan trade wameandaa mabanda ya kutosha hivyo Makampuni taasisi na wanakaribishwa kuendelea kufanya usajili .

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mwenza wa Masoko Kampuni ya Tanza Kwanza Franscis Daudi amesema katika maonyesho ya Sabasaba ya 47 kutakuwa na kujadiliana changamoto na fursa zilizopo katika sekta 8 ikiwemo Madini, Viwanda, Mazingira, Uwekezaji, na Michezo hivyo watatekeleza lengo la nchi kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Tutajadiliana fursa na changamoto zinazopatikana katika kila sekta hiyo ni kutekeleza wito wa Rais alioutoa mwaka 2022 kukutanisha sekta 8 muhimu hivyo ametoa wito kwa watu kuwasiliana uwepo wao katika mabanda Sabasaba expo village Makampuni yaliyofanya vizuri yatatambuliwa kwa kupewa cheti” amesema Francis

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Dar es salaam Yusufu Namoto amesema Wamachinga ni kundi linalothaminiwa na serikali hivyo wanatamani kwa miaka kadhaa ijayo kuondoa dhana ya machinga siyo mtu anayekaa barabarani kwani wataunganisha nguvu ya pamoja kuzalisha bidhaa na kusambazia walaji ..

Tunshukuru Rais wetu Dkt Samia Suluhu kwa kulipenda kundi hili kwani aliwapatia fursa ya kwenda nchi Rawanda kupata mafunzo ambapo walijifunza namna wenzao wanavyofanya hivyo kupitia wameandaa kituo maalumu kuongeza maarifa na kuwatafutia soko la uhakika” amesema Namoto.

Naye Mtafiti na Mgunduzi wa vyakula vya asili Kampuni ya Dorkin Profesa Dorkasi Kibona amesema wamekuwa wakihakikisha wanatumia Kilimo cha asili kuzalisha na kuchakata na wamekuwa wakipika chakula cha asili na wamebahatika kuenda kuonyeha chakula Cha kitanzani marekani na kupatiwa cheti

Tanzania tunaweza kufanya vitu vya asili na kukitangaza kimataifa sasa Kampuni hii tunalima mazao pasipo kutumia mbolea ya za viwandani hivyo kupiti hivyo vijana wa kitanzani kuchangamkia fursa ya Kilimo cha asili na Tanzania tutambue imebarikiwa udongo mzuri sana” amesema Dorcas

Naye Salim Ahmed Msanii wa filamu kwa jina maarufu (Gabo Zagambo) amesema naye atashiriki katika maonyesho hayo kwani ataonyesha filamu yake ya kipekee watu wasisubirie kuhadithiwa na anamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fursa ya kuwatambua wasanii kwa kutoa mikopo na yeye pia ni mnufaika imeimsaidia kujikwamua kiuchumi na kufanya kazi zake vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!