Na Neema Kandoro Mwanza
Wadau wa Madini wamepongeza ujio wa Waziri wa Madini Mhe Anthony Peter Mavunde alieongoza kikao kilichofanyika Mkoani Mwanza lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo sekta iyooo
Akizungumza Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Ujenzi Mjasilia Hamis Juma alisema tunampongeza Mhe Waziri wa Madini Anthony Mavunde kuweka Mikakati ya kuhakikisha 2030 wanatenga Maeneo yote nchini yanayofanyiwa utafiti na kuongeza Kasi ya Uwekezaji katika sekta ya Madini Nchin
Naye Waziri wa Madini Mhe, Anthony Peter Mavunde alisema kuwa ikiwa ni Utekelezaji wa Vision ya 2030 ya Madini ni Maisha na utajili, Wizara ya Madini Tanzania (GST) imefanikiwa kufanya utafiti wa kina na Majaribio katika Mikoa ya Dodoma Geita na eneo la kahama Lengo likiwa ni Mkakati wa kuhakikisha ifikapo Mwaka 2023 Maeneo yote nchini yanafanyiwa utafiti na kuongeza Kasi ya Uwekezaji katika sekta ya Madini Nchini
Naye Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven kiruswa ameongea kuwa Wizara ya Madini itaendelea Kutatua changamoto zinazowakumba wadau wa Madini ikiwa ni Pamoja kuhakikisha Miundombinu ya Umeme na Barbara inaboreshwa Kwa Shughuri za uchimbaji wa Madini.