Na Theophilida Felician, Kagera
Wafanyakazi pamoja na wa dau mbalimbali katika bandari ya Bukoba Mkoani Kagera wameishukuru na kuipongeza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa Kagera kwakuwafikia na kuwaelimisha zaidi kuhusu rushwa na madhara yake.
Wamezitoa pongezi hizo mara baada ya kupata somo mahususi kutoka kwa Mkuu wa Takukuru Kagera John Joseph wakati Taasisi hiyo ikiwa imetembelea Bandari hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu mpango mpya wa “TAKUKURU RAFIKI” mpango ambao unahamashishwa nchi nzima.

Wemesema kuwa kupitia somo hilo ni mambo muhimu waliyoyapata kuhusu rushwa na athari zake kutoka kwa mwezeshaji huyo Mkuu wa Takukuru John Joseph ambaye ametumia muda mwingi katika kuielezea kwa undani program hiyo.
“Tunakushukuru sana kupitia elimu hii kama itaendelea kuhamasishwa zaidi hususani katika Taasisi zetu za umma pengine tutafanikiwa kuitokomeza rushwa hii kwani huko bado hali siyo nzuri jikiteni huko sana sana”
wemesema wadau hao na wafanyakazi.
Mariko Kingunge kutokea TPA amesema elimu hii ni muhimu sana “ila ni kuombe Mkuu endelea kufanya hivyo kwa taasisi mbalimbali kwa sababu rushwa ipo kwa watu waelewa siyo kwa watu wasioelewa ipo kwa viongozi ipo kwa matajili ipo kwa wafanya biashara ipo kwa maskini ni wambieni ndugu zangu mara nyingi tumekuwa tukipeleka taarifa zetu Takukuru pindi tunapokuwa tumeshindwa kutimiza matakwa ya kufanikisha malengo yetu mnapokuwa katika makubaliano kati ya mtoa rushwa na mpokea rushwa haitolewi taarifa isipokuwa pale tuu mkiferi mtu anawahi Takukuru acheni kuwapa kazi ngumu Takukuru”amesikika Marco Rugakingira akiyasisitiza maneno hayo.
Dauda Khalfani mfanyakazi bandarini pamoja naye Hussein Salumu wameongezea wakiiomba Taasisi hiyo ifanye uhamasishaji wa mara kwa mara katika Bandari hiyo kwani nako nisehemu muhimu sana.

Naye Mkuu wa bandari hiyo Denis Mapunda ameungana na wenzake na kuishukuru taasisi hiyo kwakuitembelea bandari hiyo huku akiahindi kushiriki utekelezaji kwa vitendo elimu aliyoipata katika kutimiza wajibu wa majukumu yake pamoja na wafanyakazi wenzake.
Kwingineko John Joseph ambaye amehusika katika otoaji wa elimu kwa wadau hao ikiwa ni mwendelezo wa kuinadi programu hiyo mpya ya “Takukuru rafiki” yenye adhima ya kuwafikia wadau mbalimbali katika kupanua wigo dhidi ya mapambano ya vitendo vya rushwa amewaeleza kuwa mpango huo utawafikia watu wote kwa malengo ya kuhamasishwa zaidi nini maana ya rushwa na madhara yake.
Amefafanua kwamba katika utekelezaji wa mpango huo unaohamasishwa nchi nzima utatekelezwa kwa njia tofauti tofauti “
“Kwanza tumeanza na kutoa elimu kama hivi tulivyo hapa baadaye itafuatia hatua yakukutana tena na wadau kama tulivyo mtapewa karatasi kwakila mmoja atatuandikia kero yake moja tuu inayomsibu halafu tutaona ni kero zipi zilizozungumziwa kwa wingi tutazipigia kura mwisho wasiku tutapata kero ambazo zitakuwa ni sahihi na zitafanyiwa ufumbuzi kupitia wahusika watakaokuwa wanahusika moja kwa moja na kero hizo mfano afya, elimu, maji, umeme na nyinginezo wahusika iwe wizara, idara au mtu yoyote watahusika ili kuitatua kero hiyo na kupatiwa mwafaka thabiti “John Josph akiwaelimisha kwa mapana wadau hao.
Mbali na hayo amefafanua juu utofauti wa rushwa na hongo kwani watu wengi wamekuwa akifahamu kuwa rushwa na hongo ni kitu kimoja jambo ambalo si kweli.
Hongo ameitaja kuwa ni kitendo cha kutoa pesa au kitu chenye thamani ili ufanyiwe jambo flani, na rushwa ni upindishaji wa taratibu unaofanywa mtu mmoja au kundi la watu kwa maslahi binafsi hivyo kutokana na mambo hayo mawili yote kuwa adui wa haki amewahimiza kutambua umuhimu wa kutokushiriki kabisa masuala ya rushwa katika utekelezaji wa kutoa huduma kwa umma vinginevyo atakayeshindwa kuzingatia ushauri huo akashiriki rushwa na akabainika atawajibishwa tuu kwa mjibu wa sheria.
