Home Kitaifa MBUNGE AREJESHA TABASAMU KWA WANAFUNZI WALIOPATA AJALI YA MOTO/ WADAU WAMUUNGA...

MBUNGE AREJESHA TABASAMU KWA WANAFUNZI WALIOPATA AJALI YA MOTO/ WADAU WAMUUNGA MKONO.

Akiongea mara baada ya kufika eneo la tukio, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe. Mhandisi Ezra Chiwelesa amesikitishwa na hali aliyoikuta shuleni hapo na kuitaka jamii kwa kushirikiana na wadau pamoja na serikali kulichukulia suala hilo kama dharula na kutoa msaada wa haraka.

Katika kuhakikisha anatoa pole kwa wanafunzi na faraja, Mbunge Ezra ametoa magodoro 50 huku akiungwa mkono na mgodi wa Stamico waliotoa magodoro 50 pamoja na kampeini ya Alsamood ya wilayani Biharamulo waliotoa mashuka Zaidi ya 280 kwa wanafunzi hao.

Aidha amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kutoa msaada ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao huku akieleza kuwa kamati ya ulinzi na usalama imemteua katibu tawala wa Wilaya hiyo kuwa Mratibu na mpokeaji wa misaada hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Biharamulo Mhe Kemilembe Lwota amesema kutokana na dharula iliyopo tayari ameshatoa maagizo kuanza kwa ujenzi wa bweni hilo mara Moja na kusisitiza kuwa kufikia jumamosi ya Julai 23 Mwaka huu wanafunzi wawe wamerejea kwenye bweni hilo.

Kemilembe amewasihi wanafunzi kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki huku serikali ikishughulikia jambo lao na kuwataka Wazazi kuwa na amani kuwa watoto wao wako salama huku akieleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama bado vinafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Bweni la Wasichana katika shule ya sekondari Mubaba iliyopo kata ya Kaniha wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa kwa wanafunzi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Alfred Katobesi ameeleza kuwa Julai 17 Mwaka huu, moto huo ulianza majira ya saa 12 jioni wakati wanafunzi wote wakiwa wameenda kupata chakula Cha usiku.

Ameongeza kuwa moto huo umeteketeza Mali zote za wanafunzi yakiwemo magodoro, vitanda, nguo, Madaftari na kuwaacha wanafunzi wakiwa hawana msaada wowote hali iliyowapelekea wanafunzi hao kulala madarasani.

Kwa upande wao wanafunzi wameomba serikali kuwasaidia kwa unataka maana wao kama watoto wa kike ajali hiyo imewaathiri pakubwa huku wakishukuru kwa hatua ambazo zimeshaanza kuchukuliwa.

Wameongeza kuwa serikali iwasaidie kuwajengea Mabweni mengine ILI kupunguza msomgamano katika bweni lililouungua ambalo lilikuwa likibeba wanafunzi 135 huku uwezo wake ni wanafunzi 108.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!