Na Joel Maduka Geita.
Wadau wa sekta ya madini, wafanyabisahara na wajasiriamali mkoa wa Geita wameombwa kutumia fursa za mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha ambazo zinakuwa na riba nafuu zitakazo uwezesha Mkoa huo kuinuka kiuchumi, huku wakiondolewa hofu juu ya mikopo hiyo.
Serikali imekuwa kwenye malengo ya kuufanya Mkoa huu wa Geita kuwa kitovu cha uchumi ndani ya taifa na ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo mara kadhaa wananchi wametakiwa kutumia fursa hiyo kwenye uwekezaji kutokana na raslimali zilizopo kwenye sekta ya madini, kilimo, ufugaji na uvuvi.
Ili kufanikisha kuinua malengo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela wakati akizindua tawi la Benki ya Biashara ya Taifa (TCB) ameipongeza Taasisi hiyo ya kifedha kuwezesha mikopo kwa wananchi zaidi ya Sh. Bilioni tisa.
“Niwaombe wachimbaji wadogo nendeni mkakope Banki achaneni na Mikopo umiza ambayo inatolewa na watu Binafsi kwani ainafaida kwenu na ndio chanzo cha kuwanyonya wachimbaji wadogo” Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB Sabasaba Moshingi ametumia jukwaa hili kuishurukuru serikali kuwapa nafasi ya
kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii kuyahudumia lengo likiwa nimkuinua uchumi.
“Msiogope kukopa, haya makampuni makubwa mnayoyaona duniani ni wateja qazuri wa benki, hususani mikopo, kwa hiyo msiogope, cha msingi kopa ukiwa na sababu.Ukikopa peleka hizo fedha kwenye hiyo sababu uliyoikopea na kama ni biashara uwe umeshaifanya na kupata uzoefu, siyo unakuwa na mawazo unataka ukope, biashara hiyo inaweza ikamaliza pesa zako.” Sabasaba Moshingi Mkurugenzi Mkuu TCB.
Aidha alibainisha ndani ya kipindi cha miaka 10 (2013-2023) benki ya TCB imepiga hatua ya uwekezaji kutoka Sh bilioni 121 hadi Sh Trilioni 1.4 na kuongeza matawi kutoka 30 hadi kufikia 82.