Home Kitaifa WACHEZAJI WA YANGA : TUKO TAYARI KUHESABIWA, KWA MAENDELEO YA WANANCHI

WACHEZAJI WA YANGA : TUKO TAYARI KUHESABIWA, KWA MAENDELEO YA WANANCHI

Wachezaji wa Klabu ya Yanga, wamewasihi wapenzi wa soka nchini na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki zoezi la Sensa litakalofanyika Agosti 23, 2022.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakiwa Kambini kwao AVIC Town Kigamboni, wao kama wachezaji watamuunga mkono Rais Samia kushiriki zoezi la kuhesabiwa.

“Mimi Feisali Salum mchezaji wa Yanga, napenda kuwajulisha wananchi wote na wapenzj wa mpira wajiandae kuhesabiwa Agosti 23, 2022” – Amesema Feisali Salum

Kwa upande wake beki Mahiri wa Yanga Dickson Job amewataka vijana wote kushiriki zoezi hilo la Sensa kwa manufaa yao.

“Napenda kuwashauri vijana wenzangu, waweze kujitokeza kwa wingi siku ya Agosti 23, 2022, Sensa kwa maendeleo ya Watanzania”

Wakati huuohuo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Timu hiyo Fiston Mayele amewaasa Watanzania wote bila kujali tofauti zao mbalimbali washiriki zoezi hilo la Sensa ili waweze kupata maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!