Home Michezo WACHEZAJI BOMBOKA FC WAKABIDHIWA BIMA ZA AFYA C.H.F

WACHEZAJI BOMBOKA FC WAKABIDHIWA BIMA ZA AFYA C.H.F

Na Boniface Gideon, TANGA

Wachezaji 25 wa Timu ya mpira wa miguu ‘Bomboka Fc ‘ inayoshiriki ligi ya Mkoa wa Tanga,Leo wamekabidhiwa Bima za Afya. Bima hizo zimetolewa na Wafanyakazi wa Taasisi ya Gift of hope Foundation chini ya Mwenyekiti wa Timu Said Bandawe

Akikabidhi Bima hizo , Mustahiki meya wa Jiji la Tanga Abdarahaman Shiloo aliwapongeza Viongozi wa Timu hiyo kwa hatua kubwa waliyoifikia kwakuhakikisha wachezaji wa Timu hiyo wanakuwa na Bima za Afya.

Aliwataka Wanamichezo na Jamii kuweka utaratibu wa kukata Bima za Afya ili kuwapa unafuu wa matibabu wanapopatwa na maradhi au ajari,

“Bima hii ni Bei nafuu, ukiwa na shilingi 30,000 unauwezo wakukata wewe na familia yako mkapata matibabu katika hospitali zote za umma nchini, niwaombe Wananchi hebu tuichangamkie fursa hii” Alisisitiza Shiloo

Aliwataka Wadau mbalimbali hususani wa michezo kuhakikisha vikundi vya michezo wanakuwa na Bima za Afya ili kuwapa unafuu Wanamichezo kupata huduma ya matibabu kwa wakati,

“Hii itawasaidia Wanamichezo kupata matibabu kwa wakati na kupunguza gharama za matibabu kupitia Bima ,huu ni mfano mkubwa Sana kwa Jamii hususani Wanamichezo” Alisema Shiloo

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Timu hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Gift of hope Foundation inayotoa msaada kwa waraibu wa Dawa za kulevya Said Bandawe Alisema Bima hizo zimetolewa na Wafanyakazi wa Taasisi hiyo ikiwa ni Sehemu ya kuhakikisha usalama pale wanapopata majeraha uwanjani ,

” Tumeona namna tunavyoteseka pale wachezaji wetu wanapopata majeraha Viongozi tunachangishana hela ili tuwatibu wachezaji wetu, kwahiyo tukaona ni vizuri tuwafungulie Bima hii kwa wachezaji wetu 25 ” Alisema Bandawe

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!