– WAOMBA BODI YA BARABARA IJE NA HOJA YA PAMOJA
Na Shomari Binda-Musoma
WABUNGE kutoka mkoa wa Mara wamemshukuru na kumpongeza mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda kwa usimamizi na ufatiliaji wa miradi ikiwemo ya barabara.
Wakichangia kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji wamesema ufatiliaji wake umepelekea kuuchangamsha mkoa.
Mbunge wa viti maaum mkoa wa Mara Ghati Chomete amesema miradi ya barabara inayosimamiwa na Tanrods na Tarura mkoa wa Mara imekuwa ikiendelea vizuri na mkuu wa mkoa amekuwa akifanya ufatiliaji kwa karibu.
Amesema kazi nzuri zinazoonekana kwenye miradi ya barabara upo ufatiliaji unaofanywa na mkuu wa mkoa hivyo hakuna budi kumshukuru na kumpongeza.
Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara licha ya kumshukuru na kumpongeza mkuu huyo wa mkoa lakini amepongeza pia kazi xinazofanywa na Tanroads pamoja na Tarura kwa usimamizi wa miradi ya barabara.
Amesema kwa jimbo la Tarime vijijini upo uhitaji wa taa za barabarani hasa eneo la Komaswa ili kuweza kulinda barabara na kuwasaidia wananchi katika shughuli za kiuchumi.
Akichangia kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameiomba Tarura mkoa wa Mara kutengeneza barabara zinazoingia kwenye shule.
Muhongo ameiomba kamati ya bodi ya barabara kutengeneza hoja za barabara za mkoa wa Mara inayoeleza barabara zenye ujitaji wa lami ili kuweza kuzisemea zaidi wanapokuwa bungeni.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedatus Mathayo ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwapa kazi wakandarasi wa ndani na kuomba kupewa fedha zao kwa wakati ili kuendelea kutekeleza majukumu yao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na mbunge wa jimbo la Butiama Jumanne Sagini amesema katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka wataendelea kuwachukulia hatua madereva wanaotumia barabara vibaya ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani na kuwaondolea sifa ya kuwa na leseni.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda amesema michango iliyotolewa na wabunge Tanroads pamoja na Tarura mkoa wa Mara kuizingatia na kufanyia kazi.
Amesema barabara ni uchumi na pale zinapokuwa zinapitika kwa wakati wote uwasaidia wananchi kiuchumi.