Home Kitaifa WABUNGE MARA WAWEKA KAMBI MAJIMBONI; MUHONGO, CHOMETE KUPISHANA MUSOMA VIJIJINI

WABUNGE MARA WAWEKA KAMBI MAJIMBONI; MUHONGO, CHOMETE KUPISHANA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

WABUNGE kutoka mkoa wa Mara wameweka kambi kwenye majimbo yao na wale wa viti maalum kufatilia utekelezaji wa ilani na uhai wa chama.

Mzawa blog imekuwa ikifatilia ziara za wabunge hao na kuona namna wanavyokutana na wananchi katika kuzungumza nao namna utekeleza unavyotekelezwa na kuchangia shughuli za maendeleo.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini ameendea na ziara ya kupita kwenye Kata 16 kufatilia utekelezaji wa ilani na kuona uhai wa chama.

Katika ziara zake hizo Mathayo pia amekuwa akichangia fedha katika kuwainua wajasiliamali na vijana kupewa miradi ya ufugaji wab kuku.

Jimbo la Bunda mjini mbunge, Chacha Maboto yupo ziarani na hivi karibuni ametoa zaidi ya shilingi milioni 4 kusaidia vifaa kwa wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha 5.

Mbunge wa viti maalum, Agness Marwa kwa upande wake tayari ameshafika majimbo ya Musoma mjini na vijijini kukutana na wananchi na kutoa michango mbalimbali kwa wajasiliamali wakiwemo wanawake.

Akiwa Musoma vijiiini,A gness amechangia mifuko ya saruji kwaajili ya ujenzi wa maabara shule ya sekondari na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi 200.

Profesa Sospeter Muhongo, mbunge wa jimbo la Musoma vijijini tayari ameweka wazi ratiba ya kuanza ziara Kata 21 kukutana na wananchi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara Ghati Chomete ratiba yake itaanzia Kijiji cha Nyambono jimbo la Musoma vijijini kupishana na Muhongo kuwasikiliza wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!