Home Kitaifa WAANDISHI WATAJWA KUWA NA NGUVU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI

WAANDISHI WATAJWA KUWA NA NGUVU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI

Na Shomari Binda-Musoma

WAANDISHI wa Habari wametajwa kuwa na nguvu kubwa kwenye mapambano dhidi ya Rushwa kuelekea uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Kauli hiyo imetolewa leo agosti 9 na mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara Muhamed Shariff kwenye kikao kazi baina ya ya taasisi hiyo na Waandishi wa Habari.

Amesema Kifungu cha 7(b)kikisomwa pamoja na kifungu cha 45 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Sura ya 329) kinaitaka TAKUKURU ihamasishe ushiriki wa wadau katika kuondoa Rushwa nchini.

Amesema TAKUKURU inatambua kwamba Waandishi na vyombo vya habari vinaaminika sana katika kuhakikisha taarifa au habari muhimu sana kwa ustawi wa wananchi inawafikia

Sharif amesema Waandishi na vyombo vya habari wanashughulikia uzalendo na uhai wa nchi kwa kutoa habari za kuelimisha ,kuburudisha na kuonyesha njia.

” Waandishi na vyombo vya habari mna aminiwa sana na mnao ushawishi mkubwa kwa watanzania kwa hiyo utumieni ushawishi huo kuwaelekeza watanzania kwenye vita dhidi ya Rushwa.

” Tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na baadae uchaguzi mkuu mwakani tunaamini tutasaidiana kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya Rushwa”amesema.

Afisa uchaguzi manispaa ya Musoma Deus Nyakiriga amesema uchaguzi wa viongozi wa serikali ni hitaji la kikatiba na takwa la demokrasi.

Amesema katika kuhakikisha wananchi wanashiriki vyema uchaguzi wa serikali za mitaa watawatumia Waandishi wa Habari katika katika uelimishaji.

Takukuru mkoa wa Mara imeanza vikao vya kukutana na wadau mbalimbali kutoa elimu juu ya madhara ya Rushwa kwenye uchaguzi ikianza na Waandishi wa Habari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!