Home Afya WAANDISHI WANAWAKE MKOA WA MARA WATOA MSAADA KITENGO CHA WATOTO NJITI HOSPITAL...

WAANDISHI WANAWAKE MKOA WA MARA WATOA MSAADA KITENGO CHA WATOTO NJITI HOSPITAL YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE.

Waandishi wa Habari wanawake mkoani Mara wametoa msaada na kupata uelewa juu ya uangalizi wa watoto njiti kwenye hospital ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere.

Akizungumza hospitalini mara baada ya kukabidhi msaada kwa wazazi wa watoto hao ikiwa ni muendelezo wa sherehe za siku ya wanawake duniani mmoja wa waandishi hao Asha Shabani wa EATV amesema kama sehemu ya jamii wameamua kufika hospitalini hapo.

Amesema siku ya wanawake duniani isitumike kama sherehe ya kula na kunywa bali wakumbukwe watu wenye mahitaji, mwandishi huyo amesema kwa kufika kitengo hicho licha ya kutoa msaada wamesikia changamoto mbalimbali kutoka kwa mkuu wa kitengo hicho na kupitia taaluma yao watakwenda kuzifikisha kwa jamii.

Asha amesema moja ya changamoto ni wazazi wa watoto njiti kukaa muda mrefu wodini hivyo wanahitaji kusaidiwa ikiwa ni pamoja na maziwa ya watoto.

” Sisi kama Waandishi wa Habari Wanawake leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tumeamua kutembelea kitengo cha watoto njiti hapa hospitalini.

” Kufika hapa hospitalini kumetusadia kupata uelewa na baada ya hapa tutakwenda kutumia taaluma yetu kuzungumza na jamii”amesema Asha.

Mkuu wa kitengo cha watoto wachanga hospitalini hapo Anastera Ishengoma amesema wanapokea watoto wanaozaliwa na changamoto kutoka mkoa mzima na kuwahudumia, Amesema kwa sasa wana daktari bingwa wa watoto hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na wanatoa huduma za kibingwa kwa watoto.

Kwa upande wake muuguzi kiongozi wa zamu Mwajuma Adam amewashukuru Waandishi hao kwa kuguswa na watoto hao na kuamua kuwasaidia kupitia wazazi wao

Msaada waliotoa waandishi hao ni pamoja na maziwa ya watoto,pampas,mafuta na sabuni huku wadau wengine wakiombwa kuchangia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!