WAANDISHI wa habari wa Mkoa wa Pwani wamefanya ziara ya kutembelea kituo kikuu cha kupokelea uingizaji wa gasi ya kampuni ya Taifa Gas nchini kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam kwaajili ya Mafunzo ya siku moja kwa lengo la kuwajengewa uwezo kuhusu umuhimu wa matumizi ya gasi mbadala badala ya matumizi ya mkaa na Kuni kwa taifa.
Akizungumza na Waandishi hao wa Habari Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Taifa Gas Ambwene Mwakalinga amesema Waandishi wa Habari waandike Habari za kuelimishe jamii kuhusu Faida na umuhimu wa matumizi ya gasi mbadala kwani asilimia 98.9 ya Watanzania bado wanatumia mkaa na kuni idadi ambayo bado ni kubwa.
Amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya nishati mbadala na kuelimishwa athari za matumizi ya mkaa na kuni ambayo kusababisha ukataji miti na kuendelea kwa uharibifu wa mazingira nchini.
Lengo la ziara hiyo ni kujifunza masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati mbadala pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za uchakataji wa gesi kutoka katika kituo mpaka hatua ya mwisho ya kufika kwa jamii.
Akizungumzia mkakati wa Kampuni ya Taifa Gas iliyojiwekea katika kuhimalisha usambazaji wa gasi hiyo nchini Ambwene amesema kampuni hiyo inaendelea na uwekezaji kujenga kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa mitungi katika Mji wa Kibaha kinachotarajia kuanza uzalishaji baada ya miezi mitatu kutoka sasa.
Amesema, waandishi wa habari wanatakiwa kuchukua hatua ili kusaidiana na Serikali kuokoa mazingira hasa katika kupunguza wimbi la ukataji miti hovyo kwasababu ya kuchomea mkaa na kuni.
Aidha Ambwene amesema ili kufikia malengo ni vyema Serikali ikapandisha bei ya vibali vya uchomaji mkaa na kwamba kufanya hivyo itapunguza wimbi la watu kukimbilia kwenye mkaa na hivyo kutumia nishati mbadala kwa wingi.
+++++++++++++++