Na Shomari Binda-Musoma
WAANDISHI wa Habari Wanawake mkoa wa Mara wamepanga kutembelea na kupata uelewa namna ya matunzo na uangalizi wa watoto njiti.
Ziara hiyo itafanyika machi 9 ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo uhadhimishwa kila mwaka machi 8.
Katibu wa kikundi cha Waandishi wa Habari wanawake mkoa wa Mara Ghati Msamba amesema lengo ya ziara hiyo ni kwenda kupata uelewa na kuweza kuandika vyema juu ya changamoto za watoto hao.
Amesema waandishi wanapokuwa na uelewa mkubwa juu ya jambo fulani wanaweza kuliandikia vizuri na watu wakalielewa.
Ghati amesema watakapokutana na wataalamu wa kitengo hicho watawapa ufafanuzi juu ya masuala watakayo wauliza ili waweze kusaidia jamii.
Amesema inawezekana yupo mwanamke akapata changamoto ya kujifungua mtoto njiti akiwa mbali na huduma stahiki kama atakuwa hana uelewa hawezi kumsaidia mtoto.
” Sisi kama kikundi cha Waandishi wa Habari wanawake katika maadhimisho ya siku ya wanawake tutakwenda kutembelea kitengo cha watoto njiti hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
” Tunakwenda kupata uelewa ili tuweze kuandika na kuifahamisha jamii juu ya uangalizi wa mtoto aliyezaliwa njiti”amesema
Aidha katibu huyo amesema machi 10 nao wataadhimisha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.
Ghati amewaomba wadau mbalimbali kushirikiana nao kwa kuwa kuna elimu mbalimbali itatolewa ikiwa ni pamoja na malezi ya watoto