Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza ( MPC ) imefanya Mkutano Mkuu Maalum wa Mwaka 2022 ikiwa ni utaratibu wa kufanya mkutano Mkuu kila mwisho wa mwaka kwa kuishirikisha vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza EDWIN SOKO amesema kila mwisho wa mwaka klabu hiyo Ina utaratibu wa kufanya mkutano Mkuu .
Naye KULWA MASOLWA Mhandisi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa ( TCRA ) amewataka Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza waweze kushirikiana katika umoja wao uliopo huku akiwaomba kuendeleza ushirikiano kati ya Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza ( MPC ) pamoja na ( TCRA ).
Sambamba na hayo klabu hiyo kupitia kamati tendaji inapenda kuwashukuru wanachama wote na wadau mbalimbali ikiwemo,UTPC, EWURA, MWANZA HOTEAL,OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA, OFISI YA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA,ILEMELA, NYAMAGANA NA MAGU.