Patrick Rweshambula, mkulima wa kahawa kutoka Kagera, akikabidhiwa pikipiki kama moja ya zawadi kuu katika promosheni ya Vuna na Mixx by Yas. Akimkabidhi zawadi hiyo ni Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Mixx by Yas, akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajat Fatma Mwasa. Wakishuhudia ni Abdillah Luholela, Kaimu Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Ziwa, na DAS wa Karagwe, Nichson Frank.
Na Mwandishi Wetu.
Kagera, Tanzania – Mixx by Yas, huduma inayolenga kuimarisha maisha ya wakulima, imehitimisha kampeni yake ya Vuna na Mixx by Yas kwa kugawa zawadi zenye thamani kubwa kwa wakulima waliofanya vizuri kupitia vyama vya ushirika vya AMCOS kutoka mikoa ya Simiyu, Kagera
Katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kagera, jumla ya zawadi zilizotolewa ni pamoja na pikipiki 4, baiskeli 10, paneli za sola 3, na simu janja 6. Tukio hili limevutia wakulima kutoka AMCOS mbalimbali, viongozi wa serikali, na wadau wa kilimo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Mixx by Yas, alisema:
“Kampeni ya Vuna na Mixx by Yas ni sehemu ya juhudi zetu za kuthamini mchango mkubwa wa wakulima katika uchumi wa taifa. Tumefurahi kuwazawadia zawadi hizi muhimu ambazo tunatarajia zitachangia kuboresha maisha na shughuli zao za kilimo. Tunajivunia kuwa washirika wa karibu wa wakulima, na kupitia huduma kama KilimoPesa na AfyaMkulima, tunalenga kuwapa suluhisho bora zaidi kwa changamoto zao za kila siku.”
Mmoja wa wakulima walioshinda, Bw. Patrick Rweshambula kutoka Kagera ambaye alipokea pikipiki, alielezea furaha yake:
“Nimefurahi sana kupata pikipiki hii, itaniwezesha kusafirisha mazao yangu sokoni kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Shukrani kwa Mixx by Yas kwa kutambua na kuthamini kazi ya wakulima.”
Naye Elizabeth Gacha kutoka Simiyu, aliyeshinda paneli ya sola, alisema:
“Paneli ya sola niliyopewa itanisaidia sana hasa katika kuhifadhi mazao yangu kwa kutumia nishati ya jua. Pia, itakuwa msaada mkubwa kwa familia yangu nyumbani. Nashukuru sana Mixx by Yas kwa zawadi hii.”
Kampeni ya Vuna na Mixx by Yas si tu kwamba imeleta matumaini kwa wakulima, bali pia imedhihirisha dhamira ya Mixx by Yas ya kuleta suluhisho bunifu kwa changamoto za sekta ya kilimo. Mpaka sasa, Mixx by Yas imefanikiwa kufanya malipo ya shilingi bilioni 5.5 kwa wakulima zaidi ya 4,340 kupitia AMCOS 18 nchini.
Huduma za KilimoPesa na AfyaMkulima, zilizozinduliwa hivi karibuni, zimeendelea kuimarisha maisha ya wakulima. Kupitia KilimoPesa, wakulima wanapata mikopo nafuu kwa ajili ya pembejeo na mbolea, huku AfyaMkulima ikiwapa wakulima na familia zao bima ya afya kwa gharama nafuu.
Mixx by Yas inaendelea kuwa mshirika muhimu wa wakulima kwa kuwapa suluhisho salama, rahisi, na zenye tija kwa maendeleo yao na sekta ya kilimo kwa ujumla.