Na Magrethy Katengu
Kampuni ya line simu za mikononi Vodacom imeishukuru serikali kwa kufanya mabadiliko ya tozo ya miamala ya kutuma fedha na kutoa kwa kuwasaidia wananchi zawadi za usafiri wa vyombo vya moto ikiwemo bajaji pikipiki katika shughuli zao za kiuchumi.
Shukrani hizo zimetolewa Dar es salaam na Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani Brigiter Shirima katika Tamasha la kampeni ya M Pesa imetiki lililofanyila katika Viwanja vya Barafu vilivyopo Mburahati Jijini Dar es salaam kuwatangaza washindi wa awamu ya sita kushiriki katika kampeni Kwa kutumia huduma ya miamala ya M- Pesa kutoa pesa na kuingiziwa pesa kupitia line zao za Vodacom.
“Tunatoa zawadi kwa awamu ya sita sita kampeni tukiyoianza muda simrefu M-Pesa Imetiki hadharani kwani Kwa washindi wetu wa wiki waliotumia huduma zetu za kifedha hii ni ishara ya kutoa shukrani kwa serikali kwa kupunguza tozo za miamala hivyo nasi tunarudisha kwa Jamii” amesema Brigiter
Naye mshindi wa Bajaji Magdalena Magogo amesema siku hiyo imekuwa tofauti sana kwa kupokea zawadi ya bajaji hivyo anaamini kuwa mtu yeyote anaweza kuwa mshindi anachotakiwa ni kutumia huduma za kifedha za kampuni ya Vodacom.
Naye Sebastian Moshi mshindi wa pikipiki amesema yeye mwenyewe alikuwa hajui kama angekuwa mshindi lakini ndiyo Imetokea hivyo Jamii iachane na dhana kwamba wanapata zawadi ni watu wanaotengenezwa yeye mwenyewe hajuani hata na mtu mmoja mfanyakazi wa kampuni hiyo na walimpigia simu kumjukisha kuwa ameshinda kwa namba 100 .
Aidha wito unaendelea kutolewa na Kampuni hiyo kwa wale wote wanapenda kushiriki katika kampeni hiyo kuendelea kwani bado zawadi zitaendelea kutolewa ikiwemo nyumba,pikipiki bajaji .