Home Michezo VIWANJA SITA VYA MICHEZO VYATENGEWA BAJETI

VIWANJA SITA VYA MICHEZO VYATENGEWA BAJETI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, amevitaka vilabu vya michezo kufanya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ili kuinua michezo.

Mchengerwa ametoa kauli kwenye usiku wa utoaji wa Tuzo za Mashindano ya NBC, ya Shirikisho la soka nchini 2022.

Katika tukio hilio lililovuta hisia za wanamichezo ndani na nje ya nchi, tuzo 43 katika maeneo mbalimbali zimetolewa huku tukio hilo likirushwa mbashara kwenye televisheni na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Ninaagiza BMT na TFF wiki ijayo, ratibuni kikao na viongozi wa vilabu tulimalize suala hili. Wenzetu wanafanikiwa sana kwenye michezo kwa kuwa wanazingatia maadili” ameongeza, Mchengerwa

Pia amesema, Serikali inatarajia kujenga viwanja vya michezo ya ndani na sanaa eneo la Kawe, ambapo amesisitiza baada ya kukamilika utoaji wa tuzo kwa mwaka ujao utafanyika katika kumbi hizo za kisasa.

Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya michezo kuwa uchumi, amesema Serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kukarabati viwanja sita nchini, ambapo amefafanua kuwa lengo ni kuandaa mashindano ya soka ya AFCON.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!