Home Biashara VIWANDA VISIVYOFANYA KAZI KUTAFUTIWA DAWA.

VIWANDA VISIVYOFANYA KAZI KUTAFUTIWA DAWA.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji- Msajiri wa Hazina itapanga utaratibu bora wa kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa na havifanyi kazi vinaendelezwa na kufanya kazi ili kuongeza ajira, pato la taifa na kukuza uchumi kwa ujumla.

Aidha, ameiagiza Wakala wa Vipimo (WMA) kugagua mita zote za umeme viwandani ili kuhakikisha zinafanya kazi kwa usahihi na wazalishaji, wafanyabiashara, walaji na TANESCO wanapata haki yao sawasawa.

Ameyasema hayo Agosti 22, 2024 wakati wa Ziara yake Mkoani humo ambapo alipotembelea viwanda na kuongea na Wafanyabiara na Wamiliki wa Viwanda kwa lengo la kujionea utendaji kazi, kusikiliza changamoto zao na kuona njia bora ya kuzitata kwa kushirikiana na Taasisi nyingine husika.

Katika mkoa wa Tanga kuna viwanda vinavyofanya vizuri na vingine havifanyi vizuri. Hivyo Sijaridhishwa na viwanda vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi . Ninawashauri Wawekezaji waliochukua viwanda vilivyobinafsishwa kwa nia ya kuwekeza wawekeze na si kuvigeuza kuwa magodauni au kuwa sehemu ya kupata mikopo na kuwaacha Watanzania wakikosa ajira na pato la Taifa. ” Amesema Dkt. Jafo.

Aidha, amebainisha kuwa kwa kishirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekwzaji, Wizara ya Fedha, Msajiri wa Hazina pamoja na Taasisi za kisekta atahakikisha changamoto zilizotolewa zinafanyiwa kazi ili kurudisha hadhi ya Mkoa wa Tanga kama Mkoa wa Viwanda kama ilivyokuwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Kwa upande wa Changamoto ya umeme mdogo, Dkt Jafo amebainisha kuwa
Serikali imefanya jitihada kubwa kushughulikia changamoto hiyo na kuwa Mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) uko mbioni kukamilika na kuwa tatizo la umeme limeanza kupungua kwa kwa kiasi kikubwa.

Aidha katika ziara hiyo Waziri Jafo alitembelea Kiwanda cha sabuni cha Wilmar Tanzania Limited, Kiwanda cha nguo cha AFRITEX, Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh, Kiwanda cha unga cha Pembe Flour Mills na Kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro.

Akiwa katika Bandari ya Tanga amepongeza upanuzi wa bandari hiyo na kutoa wito kwa watumishi kurahisisha usafirishaji wa mizigo ya wafanyabiasha wa ndani na nje ya nchi kwa ufanisi ili kuvutia wawekezaji kuanzisha viwanda mkoani humo na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kutumia badari hiyo kwa kusafirisha bidhaa mbalimbali kama magari madini ya copper, mazao hususani katani na nyinginezo.

Katika hatua nyingine akiongea na Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda wa Mkoa wa Tanga, Waziri Jafo amewaahidi kuwa atashirikiana na Taasisi nyingine za kisekta kuzitatua ili kuhakikisha kiwa sekta ya viwanda na biashara inayoajili watu wengi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi inafanya kazi kwa ufanisi na kuleta mandeleo ya oijamii na ya kiuchumi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Jafari Kubecha amesema kutokana na maboresho ya mazingira ya biashara yanayofanywa na Serikali ikiwemo upanuzi wa bandari viwanda vitafufuka na biashara Mkoa wa Tanga itakuwa na kuchangia katika onhezeko la ajira na pato la taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!