Home Afya VITENGO HUDUMA YA DHARURA, “ICU” HOSPITAL YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MUSOMA...

VITENGO HUDUMA YA DHARURA, “ICU” HOSPITAL YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MUSOMA YAKAMILIKA VIFAA TIBA

Na Shomari Binda-Musoma

VIFAA tiba kwaajili ya kutolea huduma kwenye hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Musoma vimekamilishwa kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Kuwepo kwa vifaa hivyo kumewasaidia wananchi kusafiri hadi kwenye hospital ya kanda Bugando na hospital nyingine kwaajili ya kupata huduma.

Hayo yamesemwa na Dk.Helman Tesha mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa hospital hiyo kwa niaba ya Mganga Mfawidhi Dk.Osmund Dyagura katika mahojiano maalum na Mzawa Blog.

Amesema kwa sasa huduma za vipimo mbalimbali na matibabu ya kibingwa hupatikana hospitalini hapo na wananchi wanaendelea kuhudumiwa.

Dk.Helman amesema huduma kama ya upimaji wa magonjwa ya mfumo mzima wa moyo hutolewa na kutolewa ushauri wa kufuata.

Amesema kwa sasa wananchi wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo hawana sababu ya kusafiri umbali mrefu bali wafike hospitalini hapo na kutibiwa.

Tunaishukuru serikali yetu chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watanzania na kuwafikishia huduma stahiki kwenye maeneo yao.

Huduma ambazo zinapatikana kwa sasa kwenye hospital hii ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mwanzoni zilikiwa hazipo lakini kwa sasa mwanchi akifika lazima apate huduma“, amesema Dk.Helman.

Amesema vitengo vya kupokea wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi( ICU) vimeboreshwa kwa kuwekewa vifaa vyote vinavyohitajika.

Ameongeza kuwa licha ya uwepo wa vifaa tiba wapo madaktari bingwa na wauguzi ambao wanawahudumia wananchi kwa weledi mkubwa.

Kwa upande wao wananchi ambao walifika hospitalini hapo kwaajili ya kupata huduma wameishukuru serikali kwa kuwajali na kuwasogezea huduma karibu.

Wamesema vipo vipimo ambavyo mwanzoni iliwaghalimu kusafiri kwenda kuvipata lakini kwa sasa wanavipata wakiwa Musoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!