Home Kitaifa VITABU VINAVYOELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM VYAENDELEA KUSAMBAZWA

VITABU VINAVYOELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM VYAENDELEA KUSAMBAZWA

Na Shomari Binda-Musoma

VITABU vinavyoelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwenye jimbo la Musoma vijijini vimeendelea kusambazwa ili kusoma utekelezaji uliofanyika.

Vitabu hivyo viwili vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini vimeelezea utekelezaji kwa mwaka 2015-2020 na 2020-2025.

Akizungumza na Mzawa Blog mbunge huyo amesema vitabu hivyo vitaendelea kutolewa na kusambazwa hadi mwaka 2025 ili kuona yaliyofanyika jimboni.

Amesema sekta za elimu, afya,maji,miundombinu na shughuli za kiuchumi zimeelezwa namna zilivotekelezwa kwenye vitabu hivyo.

Muhongo amesema kwenye elimu yapo mengi yaliyofanyika ndani ya jimbo ikiwemo ujenzi wa shule mpya, madarasa na maabara zilizojengwa.

Amesema kwenye sekta ya maji Kata 21 na vijiji 68 vyote vimeshafikiwa na huduma ya maji na ipo miradi ambayo inaendelea ya kutoa maji ziwa Victoria.

Tumeeleza mengi mbayo ni utekelezaji kwenye jimbo ambayo tumefanikiwa kufanya ili kuwapatia wananchi huduma.

“Tumeongeza shule mpya kuanzia shikizi,msingi na sekondari yakiwemo madarasa mapya ambayo yamefanikisha wanafunzi kusoma bila kubanana”, amesema Muhongo.

Amesema vitabu vitasambazwa Kata zote kwa viongozi na wananchi ili kupitia na kuona namna utekelezaji wa ilani ulivyotekelezwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!