Home Kitaifa VIONGOZI WALIOCHAGULIWA WAMETAKIWA KUENDELEA KUJIFUNZA MAADILI MEMA

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA WAMETAKIWA KUENDELEA KUJIFUNZA MAADILI MEMA

Wajumbe wa mkutano mkuu wa chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi Ccm mkoa wa Dodoma wamefanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa chipukizi wa mkoa huo Patricia Evarist Paschal ambaye ameibuka kidedea kwa Kura 31 kati 41 huku wakiwataka viongozi waliochanguliwa kuendelea kujifunza maadili mema ya chama ili kuwa viongozi bora hapo baadae.

Akizungumza kwaniaba ya jumuiya hiyo Desemba 16,2023 Jijini Dodoma msimamizi mkuu wa uchanguzi ambaye pia ni katibu wa UVCCM Wilaya ya Kongwa Emanuel Msemwa amesema Chama Cha Mapinduzi kimeanza utaratibu wa kuwaandaa viongozi wa chama na serikali kuanzia ngazi ya chini kwakuwa  msingi mzuri wa kiongozi bora huanzia utotoni hivyo ni vyema wazazi na walezi kuendelea kuwalea katika misingi imara.

Wito wangu kwa waliochangulia la kwanza waendelee kujifunza maadili mema ya Chama cha Mapinduzi kwasababu bado ni watoto na ndo tunaendelea kuwalea kuja kuwa viongozi kwahiyo tuwalee pia na sisi tunaowasimamia katika misingi ya maadili ili waje wawe viongozi wazuri kama hadhima yao ambayo wenyewe wanakusudia huko mbele ya safari,”.

Lakini zaidi ya yote waendeleze juhudi katika masomo kwa sababu ni wanafunzi bado wanandoto ya kupata taaluma, waendelee kusoma kwa juhudi kwa sababu tunakoelekea elimu pia ni chanzo kikubwa sana cha maalifa,”

Naye katibu hamasa Mkoa wa Dodoma Stella Mkisi amesema kuwa  lengo lingine la chipukizi ni kuwafundisha ,uzalendo ukakamavu  ,nidhamu pamoja na kuwafundisha  historia ya chama na nchi.

Nitoe wito kwa wazazi wengine kipindi kinachokuja wanaposikia nafasi hizi zinatangazwa wawaruhusu watoto wao kugombea maana ni msingi mzuri sana kwa kijana kuingia ndani ya Chama tena Chama kikubwa kama Chama Cha Mapinduzi kwa sababu tunaanza kuwatengeneza kufahamu uongozi tangia wakiwa wadogo lakini tunawafundisha historia ya Chama na yataifa lao,

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya aliyechaguliwa Patricia Paschal, ameahidi kuwasaidia watoto wenzake kuepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia  na kuwafanya wawewazalendo na kuipenda  nchi yao.

Viiongozi waliochanguliwa katika mkutano huo ni pamoja na mwenyekiti wa Chipukizi wa Mkoa wa Dodoma Particia Paschal aliyepata kura 31 kati ya 41 , Wajumbe kamati ya uendeshaji chipukizi Mkoa wa Dodoma Shamimu Omary Haji, John Richard, Messe Raphel na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa Jesse Mhilu kwa kura 24 kati ya 41.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!