Home Kitaifa VIONGOZI WA DINI YA KIISLAM NCHINI WAELEZA DHANA YA SENSA NA KUWATAKA...

VIONGOZI WA DINI YA KIISLAM NCHINI WAELEZA DHANA YA SENSA NA KUWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUHESABIWA

Viongozi wa dini ya kiislam nchini wameungana na serikali pamoja na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuunga mkono zoezi la Sensa ya watu na makazi nchini inayotarajiwa kufanyika mnamo Agosti 23, 2022.

Kauli za viongozi hawa inakuja siku chache kabla ya zoezi la kuhesabiwa kwa wananchi wote nchini ambapo elimu na na hamasa imeendelea kutolewa kwa wananchi kushiriki ipasavyo licha ya kuwepo kwa elimu potofu kutoka kwa watu wachache juu ya dhana ya Uislam kutokubali kuhesabiwa.

“Vitabu vitakatifu vinatueleza kuwa katika sisi kila kitu unachokiona vimeiumbwa katika mpango, maana ya mipango ni uratibu mzuri wa masuala mbalimbali, na zoezi la Sensa linaafikiana kabisa na dhana ya mipango iliyo katika kitabu chetu tukufu”. Anasema Sheikh Mussa Yusuph Kundecha.

Nae Sheikh Khamis Mataka Mwenyekiti Halmashauri Kuu ya Taifa Bakwata ameongezea kwa kusema, “Sensa ni nyenzo ya kupanga maendeleo, haiwezekani kupanga maendeleo ya watu usiowafahamu idadi, hata mtume wetu Muhammad SAW alifanya Sensa alipotaka maswahaba wampe hesabu ya watu ambao wametamka shahada”

Viongozi hao ambao wameelezea chimbuko la zoezi la Sensa kwa dini ya kiislam wametaja namna sensa iliratibiwa kwa viongozi wakuu wa dini hiyo enzi na enzi na kwamba ina manufaa hata sasa kwa nchi yetu.

Sheikh Hillary Makarani almaarufu Sheikh Kipoozeo amewakumbusha waumini wa dini ya Kiislam kuwa inatakiwa hata chakula kipimwe, na kipimo ndio maana ya dhana ya Sensa.

“Sensa si jambo geni katika Uislam, Mtume SAW alituasa tupime mpaka vyakula ili tufanye vitu kwa vipimo, hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa kwa sababu za maendeleo na tumuunge mkono Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.” – Sheikh Kipoozeo.

Viongozi wengine wa dini ya kiislam ambao wameungana kwa kauli moja katika zoezi la Sensa Agosti 23, ni pamoja na Sheikh Mohammed Idd Mohammed, Imam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Risaalah Islamic Foundation pamoja Tariq Othman Twaha ambao kwa pamoja wamewaasa waislam wote kukaa mbali na kauli na upotoshaji juu ya zoezi la Sensa na kujitokeza kuhesabiwa bila kukosa.

Mwiaho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!