Home Kitaifa VIONGOZI WA DINI MARA WARIDHIA KUSHIRIKIANA NA TAKUKURU KUPINGA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI

VIONGOZI WA DINI MARA WARIDHIA KUSHIRIKIANA NA TAKUKURU KUPINGA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI

Na Shomari Binda-Musoma

VIONGOZI wa dini mkoa wa Mara kupitia kamati ya amani na maridhiano wamesema wapo tayari kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) kwenye uchaguzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao kilichofanyika leo agosti 13 kwenye ofisi za TAKUKURU na kuwashirikisha viongozi wa dini,wazee na maafisa wa taasisi hiyo wamesema kikao hicho kimekuja wakati muafaka.

Wamesema suala la Rushwa linakatazwa hata kwenye vitabu vya dini na wao wapo tayari kuwahubiria waumini juu ya athari za Rushwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano ya viongozi wa dini mkoa wa Mara Jacob Rutubija ameishukuru TAKUKURU mkoa wa Mara kwa kuwaona viongozi wa dini kuwa wanayo nafasi kubwa kwenye mapambano dhidi ya Rushwa.

Shekh wa mkoa wa Mara ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amesema viongozi wa dini wanao watu wengi na ujumbe watawafikishia juu ya athari kwenye uchaguzi.

Kiongozi wa itifaki wa kamati ya amani na maridhiano mkoa wa Mara Askofu Daniel Ouma amesema Rushwa au ufisadi ni kutotii mamlaka ya Mungu na ni dhamirio la dhambi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa kiislamc( JUWAKITA) mkoa wa Mara Asha Muhamed amesema Wanawake ni washiriki wakubwa wa uchaguzi na wanakwenda kuwapa elimu juu ya athari za Rushwa.

Mwenyekiti wa baraza la wazee manispaa ya Musoma Constantine Manjebe amesema TAKUKURU inapaswa pia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kwenda pamoja kwenye mapambano dhidi ya Rushwa kwenye uchaguzi.

Akiwasilisha mada juu ya uchaguzi kwenye kikao hicho afisa wa uchaguzi manispaa ya Musoma Deus Nyakiriga amesema uchaguzi ni takwa la kikatiba na wanao chaguliwa lazima wawajibike kwa wananchi.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuhubiri suala la amani wakati wa uchaguzi kwa waumini na kushiriki uchaguzi kwa kuwachagua viongozi wanao wataka.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara Muhamed Sharif amesema lengo la kukutana na viongozi wa dini ni kuweka mkakati wa pamoja kwenda kuzuia na kudhibiti vitendo vya Rushwa kwenye uchaguzi.

Amesema viongozi wa dini wanayo nafasi ya kukutana na waumini kwenye misikiti na makanisa baada ya swala na ibada ili kuwakumbusha madhara ya Rushwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!