Na Shomari Binda-Musoma
VIONGOZI 64 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake kutoka Wilaya ya Musoma mjini wamemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kwa kuwawezesha kupata mafunzo Veta
Mafunzo kwa viongozi hao yaliyofanyika kwa siku 5 na kuhitimishwa leo yamekuja baada ya kukabidhiwa pikipiki na chama makao makuu kwaajili ya shughuli za chama
Katibu wa CCM Kata ya Mwigobero Salum Ally amesema mafunzo hayo yameweza kuwasaidia mambo mbalimbali ya barabarani ambayo yamewasaidia kuendesha salama.
Amesema yapo mambo ambayo walikuwa hawayaelewi na sasa kupitia mafunzo hayo wameweza kuyaelewa vizuri.
“Awali tukishukuru chama makao makuu kwa kuweza kutoa pikipiki ili zitusaidie kwa shughuli za chama za kila siku”
“Tumshukuru pia mbunge wa jimbo letu la Musoma mjini Vedastus Mathayo kwa kutuwezesha kuweza kupata mafunzo Veta ya kuweza kupata uelewa zaidi wa matumizi” amesema
Salum amesema baada ya kupata mafunzo hayo kwa wale ambao hawana leseni yatawasaidia kuipata TRA na kukamilisha taratibu zote za matumizi ya chombo.
Katibu wa mbunge huyo Christopher Majala ambaye amekuwa akifatilia mafunzo hayo kwa karibu amesema viongozi hao wameyafurahia mafunzo hayo ya darasani na vitendo.
Amesema mbunge Mathayo ambaye kwa sasa yupo kwenye vikao vya bunge aliamua kuwezesha mafunzo hayo ili watumie vyombo hivyo kwa usalama zaidi.