Na Shomari Binda-Musoma
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya Musoma mjini wamekuwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza kushiriki mazoezi ya” jogging” yaliyoandaliwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka.
Mazoezi hayo yamefanyika leo septemba 28 yaliyoanzia na kumalizikia kwenye uwanja wa posta ambapo licha ya viongozi hao makundi mbalimbali yameshiriki.
Akizungumza mara baada ya mazoezi hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Benedict Magiri amemshukuru na kumpongeza mkuu huyo wa Wilaya kwa kuanzisha utaratibu huo muhimu kwa afya.
Amesema mazoezi yana umuhimu mkubwa katika kufanya mwili kuwa na afya njema na kuweza kutekeleza vyema shughuli za kiuchumi.
Magiri amesema ilani ya uchaguzi ya CCM inazungumzi pia ushiriki wa michezo na wao kama viongozi wanamuunga mkono kwa kuhamasisha wanachama na wananchi kushiriki mazoezi na michezo.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma kwa upamde wake amesema anataka Musoma iliyochangamka kwa matukio ya mara kwa mara yakiwemo ya kimichezo na burudani.
Amesema mazoezi hayo ya mbio za polepole na michezo mingine itakuwa endelevu na kuhimiza kila mmoja kutoa ushirikiano kwa kushiriki kila yanapo fanyika.
Chikoka amewashukuru viongozi wa CCM na wadau wengine kwa kujitokeza kushiriki huku akitoa msisitizo kwa watumishi wa umma kutokubaki nyuma kwenye ushiriki.
Mkuu huyo wa Wilaya amemshukuru pia mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo licha ya kutoshiriki mazoezi hayo kutokana na majukumu lakini amechangia kupatikana kwa maji ya kunywa kwa washiriki.
Jumamosi ijayo ya oktoba 5 imetangazwa na mkuu huyo wa Wilaya kuwa siku maalum ya bonanza kubwa litakaloshirikisha michezo mbalimbali na kutoa wito kwa kila mmoja kujiandaa