Home Burudani VIKUNDI 32 KUNOGESHA TAMASHA LA 13 LA MUZIKI WA KIGOGO 2022

VIKUNDI 32 KUNOGESHA TAMASHA LA 13 LA MUZIKI WA KIGOGO 2022

Na: Mwandishi Wetu, Chamwino.

ZAIDI ya vikundi 32 vya Sanaa ya ngoma vinatarajia kushiriki Tamasha la msimu wa 13 la muziki wa Wagogo (Cigogo Music festival),litakalofanyika Julai 23-24, Chamwino.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center- CAC), Bw. Frank Mgimwa, alibainisha kuwa, tayari maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa,

Mgimwa amevitaja vikundi hivyo kuwa, ni pamoja na:

“Kikundi cha: Nyota Njema, Sinai, Nyerere, Yeriko,Chibibi, Ushirikiano na Yerusalemu vyote kutoka Wilaya ya Chamwino.

Vingine ni: Nyota Njema na Ndagwa vyote kutoka Msanga, pia kundi la Mama Jusi (Chilonwa), Mch.Mwema (Nzali), Jembe (Bwawani/Chalinze),  Nuru (Mlebe), Mwenda pole (Buigiri), 

Pia vipo Juhudi, Tumaini (Kawawa),  Inueni mioyo (Msamalo), Safina (Msanga), Ufunuo (Mlimwa), Nyemo (Mapanga), Dudu Baya (Chilonwa), Sayari (Membe), Swala (Mkoyo), Faru (Songambele),  Nyota Lamali (Majeleko), 

Vikundi vingine ni Nyati (Nzali), Muungano (Singida), Kipauli-Njombe (Njombe), Hiyali ya moyo (Dodoma Jiji),  Afrika Bati (Morogoro), Fountain Gate Academy (Dodoma Jiji),  na Ilula (Iringa).

Aidha, amesema kuwa, vikundi hivyo vitapamba kwa burudani mbalimbali kwa siku zote mbili.

“Hadi kufikia Julai 22, 2022 vikundi vyote vitakuwa vimefika hapa Chamwino Ikulu Vijijini,

Na Tamasha litapamba moto kwa siku mbili, Julai 23-24, watu wote wanakaribishwa hakuna kiingilio, ni bure.” Alisema Mgimwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!