Home Kitaifa VIJIJI 3 VYA BWASI, BUGUNDA NA KOME MUSOMA VIJIJINI KUPATA MAJI YA...

VIJIJI 3 VYA BWASI, BUGUNDA NA KOME MUSOMA VIJIJINI KUPATA MAJI YA BOMBA HIVI KARIBUNI

Na Shomari Binda-Musoma

VIJIJI 3 vya Bwasi,Bugunda na Kome vilivyopo Kata ya Bulinga jimbo la Musoma vijijini vinatarajiwa kupata maji ya bomba kutoka ziwa victoria hivi karibuni.

Upatikanaji wa maji kwenye vijiji hivyo imeelezwa ni kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) wilaya ya Musoma.

Taarifa iliyotolewa na mbunge wa jumbo la Musoma mjini imesema Kata 21 yenye VIJIJI 68 vyenye Vitongoji 374, Vijiji vyote vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Ameaema maji ya bomba kutoka ziwa Victoria kwenda vijiji hivyo yatapitia bomba la Bujaga-Bulinga -Bukungu na mashine ikijengwa Kijijini cha Bujaga

Muhongo ameda tenki la ujazo wa lita 200,000 limejengwa Kijijini cha Busungu na lingine la lita 150,000 limejengwa Kijijini cha Bulinga ili kufikisha maji hayo.

Amesema maji kutoka kwenye matenki hayo pia yanasambazwa kwenye Vijiji vya Bukima Kata ya Bukima na Kwikerege Kata ya Rusoli.

Mbunge huyo amesema upanuzi unafanyika ili maji ya bomba la Bujaga-Bulinga-Busungu yasambazwe na kutumiwa kwenye Kata ya Bwasi yenye Vijiji vitatu vya Bugunda, Kome na Bwasia ambapo gharama za meadi ni shilingi milioni
997,714,196 huku urefu wa mtandao ukiwa kilomita 31.5 huku vitekea maji vikiwa 35.

Mradi huu umepangwa kyfanyika mwishoni mwa mqezi juni huku wananchi wakianza kupata maji.

Wananchi wa vijiji hivyo wametoa shukrani kwa serikali inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusambaza maji safi na salama ya bomba vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!