Vijana wa kitanzania waliokataliwa na wazazi wao wametakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili waweze kuzifikia ndoto zao
Hayo yamesemwa leo Mei 29, 2024 na Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Mapung’o Paschal katika kikao cha kusikiliza kero za makundi mbali mbali kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita
Amesema hakuna haja kwa kijana aliye na maisha ya chini kukata tamaa ya maisha yake na kushindwa kujituma katika kutafuta mali kwani hakuna aliyezaliwa akiwa na mali.
Mapung’o alisema vijana waliokumbana na kadhia hiyo kwenye maisha yao wanatakiwa kumuomba Mungu kila siku na wafanye kazi bila ya kuchagua shughuli ya kufanya ili wapate maendeleo.
Alisema yeye ni mhanga aliyekataliwa na wazazi wake lakini alijipa moyo wa kujituma na kwa sasa anajishughulisha na uchimbaji madini katika maeneo yenye leseni za uchimbaji madini akilipa kodi kwa serikali kama inavyotakiwa.
Mafung’o alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeanzisha utaratibu mzuri ambapo wafanyabiashara wanayo fursa ya kupata mikopo ya kuendeshea shughuli zao hivyo watumie mwanya huo kuinua hali zao za kimaisha.