Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Kenani Kiongosi amewataka vijana kuhamasisha zoezi la sensa na kutoa elimu ili iwe rahisi kufanikisha zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.
Amezungumza hayo wakati wa ufunguzi wa uhamasishaji wa sensa kwa vijana ambapo kila kiongozi wa vijana Mkoa ahakikishe wanahamasisha jamii kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.
Pia Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa anayewakikisha Vijana Hadija Ally Ismail amewataka vijana wajiandae na wawe mstari wa mbele kujitokeza kuhesabiwa.
“Tukijitokeza wote kuhesabiwa ili kuisaidia Serikali kuwa na Takwimu sahihi za idadi ya watu iwe rahisi katika utoaji wa huduma za jamii “amesema Hadija.
Sanjari na hayo Katibu Mkuu Umoja wa Vijana Mkoa wa Dodoma Junior Matukuta amesema wapo tayali kuhesabiwa wataende kuhamasisha wakazi wa Dodoma hasa vijana ili ujumbe uweze kufika kwa urahisi zaidi.
Vilevile amewataka vijana kujitokeza kuchukua fomu “tarehe 2 mwezi julai tunaanza kutoa fomu kuanzia ngazi ya wilaya tujitokeze kwa wingi ili tupushi ajenda za chama “amesema Matukuta.