Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii Fatuma Hassan Toufiq amewataka vijana waliopata mafunzo ya Uanagenzi Veta kuhakikisha wanayatumia katika kuwaletea tija katika shughuli hizo za ufundi stadi.
Rai hiyo imetolewa Jiji Mwanza na Mwenyekiti wa kamati hiyo Fatuma Hassan Toufiq wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa mafunzo ya ujuzaji ujuzi kwa njia ya uanagenzi unaotekelezwa na Veta kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu.
Aidha Toufiq amewataka vijana hao kuhakikisha wanayatumia vema mafunzo hayo kwa kuachana na mambo yote yanayofanya kushindwa kuyafikia malengo ambayo wameyakusudia katika mradi huo.
Mafunzo hayo mbalimbali ya ujuzaji na ujuzi yanafanyika kwa muda wa miezi nane yakiwa ni kozi ya ufundi umeme,Selemala,Bomba pamoja na ufundi wa viwanda vya kuchakata zao la pamba hadi hivi sasa wameweza kupatia mafunzo hayo kwa kipindi cha miezi miwili.
Nao baadhi ya vijana wanaopata mafunzo hayo wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fursa hiyo muhimu ambapo wamesema baada ya mafunzo hayo wanatajia kujiajiri ili kuweza kujikimu katika maisha yao.
Hata hiyo wameiomba Serikali kuwasaidia vifaa vya kazi za ufundi stadi kwa fani hizo mbalimbali walizojifunza ili utekelezaji wa sbughuli hizo za uanagenzi ziweze kufanyika kwa ustadi wa hali ya juu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA ) CPA Antony Mzee Kasore amesema,mafunzo hayo yatawasadia vijana katika kupata ajira na kuwawezesha kwenda kufanya shughuli mbalimbali ambazo zitawaingizia kipato.
“Kama tunavyokumbuka Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoingia madarakani moja ya eneo ambalo amekuwa akiliwekea msisitizo ni vyuo vya ufundi stadi nchini na vimejengwa kweli na kwasasa tuna vyuo tumejenga katika wilaya mbalimbali na kuna wilaya 64 ambazo ujenzi unaendelea ikiwemo chuo kimoja cha Songwe”
Aidha amesema ifikapo elfu 2025 Tanzania nzima kila Wilaya kuna kuwa na chuo cha ufundi stadi ili kuwasaidia vijana wengi katika kupata mafunzo ya ufundi stadi na waweze kushiriki katika miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa hapa nchini ikiweo uwekezaji unaofanywa na kuitaji vijana wenye nguvu kazi.