Na Scolastica Msewa, Kibaha
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewataka vijana wanaoibukia katika nafasi za uongozi nchini, kujadili namna ambavyo taifa na bara la afrika linawezaje kuondokana na umaskini na utegemezi wa kiuchumi.
Profesa Mkumbo, alitoa Rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku sita ya vijana viongozi zaidi ya 60 kutoka nchini Tanzania na nchi ya Afrika kusini, katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Alisema ni wajibu vijana kujifunza namna ambayo itasaidia Bara la Afrika na nchi yetu kwa ujumla kuondokana katika wimbi la umaskini na kujitegemea na kuingia katika nchi zenye ustawi mzuri wa uchumi.
Profesa Mkumbo alisema uongozi wa Karne ya 21 umejikita katika ukombozi wa kiuchumi jambo litakalo saidia wananchi kutapa kipato Kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa Kwa ujumla na kwamba viongozi vijana wanapaswa kutafuta mbinu za kuondoka katika umaskin na utegemezi.
“Katika uongozi wa Karne ya 21 , huko tulipitoka tulikazania suala la ukombozi wa kisiasa lakini mkazo mkubwa katika ulimwengu wa Leo lazima tuweke mkazo katika suala la ukombozi wa kiuchumi maana tunahitaji watu wetu wapate kipato na kazi” alisema
Mbali na hilo alisema kiuongozi kuwa Bora ni lazima awe amejijengea msingi na maarifa makubwa zaidi ya wale anaowaongoza hatua ambayo itasaidia kutatua changamoto zinazowakabili anaowaongoza
“Nimepata nafasi ya kufungua mafunzo kati ya vijana viongozi wa kitanzania na wananchi ya Afrika kusini, vijana hawa ndo wanaibuka katika uongozi, nimewasisitiza kuwa kiuongozi lazima awe na maafifa ya kujifunza Kwa kusoma” alisema
Naye Mkuu wa shule ya uongozi Ya Mwalimu Julia’s Nyerere, Profesa Mercelina Chijoriga, alisema mafunzo hayo yanatolewa Kwa vijana waopo katika sekta zilizo rasmi na zisizo rasimi ambapo watajifunza mambo mbalimbali ikiwemo kuleta mapinduzi chanya katika uchumi wa Bara la Afrika.
“Tutawafundisha vijana namna ya kutumia mafunzo hayo kuleta mabadikiko makubwa katika uchumi maana tukitazama bara la afrika linaraslimali nyingi Ila bado watu wake ni maskini …wanasema pato limeongezeka lakini ukweli ni kwamba linakuwa Kwa mtu mmoja na sio wote” alisema
Naye mnufaika wa mafunzo hayo, Bernad Gatty ambaye ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo na mbinu mbadala la kupambana na umaskini kupitia raslimali zilizopo nchini na Bara la Afrika Kwa ujumla.