Home Michezo VIJANA MOSHI VIJIJINI WAASWA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO.

VIJANA MOSHI VIJIJINI WAASWA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO.

Na ashrack miraji.

Mdau wa maendeleo Kutoka Jimbo la Moshi vijijini Enock Koola amewasihi vijana kuchangamkia fursa ya michezo kwani michezo ni ajira.

akizungumza na kituo hiki akiwa na wanachama wa simba wakifanya shughuli Mbalimbali za kijamii kufanya usafi maeneo ya Mji mdogo wa himo Mkoani Kilimanjaro Koola amesema michezo ni ajira hivyo ni vyema vijana wakatumia fursa hiyo katika kujiajiri.

“Nichukue fursa hii kuwaomba vijana wote hapa Nchin na Mkoa wetu wa Kilimanjaro kupenda Kushiriki Katika Michezo maana michezo ni Ajira na inalete mahusiano mazuri kwenye Taifa letu Leo tunamuona Mhe Rais wa jamuhur ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara na muhamasishaji mzuri Katika timu zetu za Tanzania na Sisi ni mashuda hivi karibuni tulikuwa na timu zetu hapa Tanzania Simba Day na yanga Day lakini Mhe Rais yupo kwenye ziara ametenga muda kuzungumza na timu zote mbili kuzipa hamasa kwenye Mashindano Yao huu ni uzalendo”
” amesema Enock koola”

Sambamba na hayo Koola akiwa na Viongozi wa tawi la Simba ametumia fursa hiyo kwenda kutembelea wagojwa kwenye kituo Cha Afya Himo maarufu kama OPD kugawa mahitaji muhimu Kwa wagojwa na kuwapa faraja wagojwa hao Sambamba na kufatilia huduma zinazotolewa Kwa watabibu wa kituo hicho

Hata hivyo koola ameendelea kusema hii siyo Kwa Simba pekee hata yanga wameniamba kwenda kudhamini shughuli za tawi ambalo lipo jirani na tawi la Simba hii inaonyesha kwamba michezo siyo vita au kuvunjisha amani michezo inatujenga Kwa pamoja na kutupa mafanikio Zaidi Kwenye Taifa letu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!