Home Kitaifa VIJANA JITOKEZENI JULAI 6,2024 KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI FURSA UWANJA WA MKAPA

VIJANA JITOKEZENI JULAI 6,2024 KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI FURSA UWANJA WA MKAPA

Na Magrethy Katengu– Dar es salaam

Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa Jokate Mwegelo ametoa wito kwa vijana wote Nchini kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni inayohusu fursa zilizotengenezwa na zinazotengenezwa kwa vijana nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 4, 2024 jijini Dar es salaam Joketi amesema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Julai 6, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

” Kampeni hii kubwa ina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki shughuli za kisiasa , kujiandikisha daftari la kudumu la wapiga kura litakalozinduliwa Julai 25 mwaka huu mkoani Kigoma” amesema

Nakuongeza kuwa “Kampeni hiyo itazinduliwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Balozi Emmanel Nchimbi,hivyo vijana wote wajitokeze siku hiyo ili kufahamu fursa zilizotengenezwa chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha ameongeza kuwa vijana ni wabunifu na wenye kuleta mawazo mapya ya kuinua na kuendeleza uchumi wa Taifa letu hivyo kupitia kampeni hii itasaidia kujadili fursa mbalimbali zinazowahusu vijana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!