Home Kitaifa VIJANA 3095 WAMEHITIMU MAFUNZO KATIKA JESHI LA ULINZI WA WANANCHI (JWTZ) RTS...

VIJANA 3095 WAMEHITIMU MAFUNZO KATIKA JESHI LA ULINZI WA WANANCHI (JWTZ) RTS KIHANGAIKO MSATA MKOANI PWANI

Na Scolastica Msewa, Msata.

Vijana 3095 waliohitimu mafunzo katika shule ya awali ya kijeshi ya Kihangaiko Msata Mkoani Pwani na kuwa Askari wapya wa jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania JWTZ ambao wanatarajia kusambazwa vikosi mbalimbali nchini kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa watu na mali zao.

Akizungumzia mara ya askari hao wapya kula kiapo cha utii kwa niaba ya mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania Meja Jenerali Jacob Mkunda Mkuu wa Utumishi wa jeshi la ulinzi la wananchi Meja Jenerali Marco Gaguti anawasisitiza kuzingati utiii na kanuni za kijeshi na kuheshimu maelekezo yote nayotolewa na viongozi wa nchi na kulinda afya zao na kuwataka kuishi katika kiapo, kutii maelekezo ya viongozi pamoja kutokujihisisha na vikundi vya vyama vya siasa.

“Nichukue fursa hii niwaambie au kuwakumbusha yale ambayo jeshi limetilia msisitizo leo mnahitimisha mafunzo ya askari wapya katika shule hii ya kihangaiko mnakuwa Askari wapya wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania, jeshi ambalo Lina maadili na miiko yake”

“Kazi kuu ya jeshi ni ulinzi wa mipaka ya bungeni na ni ulinzi na usalama wa jamhuri ya muungano wa Tanzania nataka kuwakumbusha kwamba jasho lenu na kazi yenu ni kwa ajili ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati huo katika maisha yenu mkumbuke hilo kwa Kila mnalolifanya jasho lako na kazi Yako ni kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania na wakati wote niwatake na niwasihi muishi kulingana na kiapo mlichokula Leo”

“Kiapo chenu katika maisha yenu wakati wote kama jeshi mfanye vizuri na kuendeleza kuwa katika weredi Ili tuweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika suala zima la ulinzi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati wote nchi yetu imekuwa nchi ya Amani na tuendelee kutoa mchango mahiri kote barani Africa kuhakikisha kwamba nchi inapata utulivu sana kupitia jeshi la ulinzi la wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania”

Amesema Askari hao wapya wakashirikiane vizuri na jamii na kutii maelekezo ya viongozi pamoja hasa Amri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan na kutojihusisa na vitendo vya uhalifu na masuala yeyote ya kisiasa.

“Jukumu letu ni kuhakikisha tunaendelea kutimiza wajibu wetu Ili nchi yetu izidi kuwa na Amani na izidi kupiga hatua za maendeleo katika nyanja mbali mbali muwe ni jeshi la kuzingatia maadili na miiko yote ambayo mmefundishwa jeshi ni sehemu ambayo nidhamu ni kipaumbele”

“Mmekula kiapo ambacho mtaishi nacho katika maisha yenu yote kama Askari wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ni wajibu wetu kumtii Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu tuna wajibu wa jeshi letu kulilinda kupitia katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania”

Meja Jenerali Marco Gaguti amewasisitiza askari hao kutii kanuni za kijeshi pamoja na kuwa walinzi wa nchi sambamba na kuwataka kulinda afya zao.

“Nitaomba muendelee kutunza afya jeshini afya ni msingi mkuu kwa utimamu na utayari wa jeshi lote hivyo kila mtu ana wajibu wa kutunza afya yake Ili jeshi liweze kunufaika kwenye utendaji wako wa kazi”

Kwa upande wake kaimu mkuu shule ya awali ya mafunzo kijeshi ya kihangaiko msata pwani Meja Haji Suluhu Haji anaeleza idadi ya vijana waliofanikiwa kuwa askari wapya wa jeshi JWTZ ikiwamo walishindwa kufanikiwa kufikia mwisho kutokana na sababu mbalimbali.

Meja Haji Suhulu Haji amesema kuwa, lengo la mafunzo ya awali ya kijeshi kwa askari hao ni kuwa watiifu, waaminifu na hodari katika ulinzi wa Taifa.

Amesema mafunzo haya ya kijeshi yamelenga kutimiza kuwa waaminifu, waadilifu, kuwa mahodari, katika kujenga Taifa kwa Amani kiakili kimwili na kujiamini kuweza kupokea amri zinazotolewa na kufuata kanuni na taratibu zilizopo katika jeshi la ulinzi la hapa Tanzania.

Amesema vijana hao wamefundishwa masomo mbali mbali na kufanya mazoezi ya michezo ili kufanikisha lengo hilo Ili kuwa na uhakika kuhusu ufaulu katika viwango vya uhakika shule ina mfumo mzuri wa upangiliaji mfumo

Awali askari hao wapya wa JWTZ walifanya maonesho mbalimbali waliopatiwa shuleni hapo ikiwamo namna ya kukabiliana na adua katika eneo la vita na mazoezi ya kuhimiri maadui.

Wanafunzi 11 waliachishwa kwa sababu ya ugonjwa kuhusu idadi 21 waliomba kuacha mafunzo wao wenyewe kuhusu 43 wameapishwa mafunzo kwa sababu ya nidhamu na kuhusu idadi 11 kwa kushindwa kupitia viwango vya mafunzo inavyostahiki na kuhusu wanne walifariki dunia mwezi June walazwe mahali pema peponi ambapo kati yao wanaume idadi 2445 na wanawake 650.

Askari 3095 wamehitimu mafunzo hayo ya awali ya kijeshi ambao ni kundi la namba 42 kwa mwaka 2020-2023 wakiwa tayari rasmi kutumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.
++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!