Home Kitaifa HAKUNA MRADI UTAKAO SIMAMA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA: BASHUNGWA

HAKUNA MRADI UTAKAO SIMAMA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA: BASHUNGWA

Karagwe – Kagera

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amewahakikishia Wananchi wa Mkoa Kagera kuwa Miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano inaendelea kutekelezwa na hakuna mradi utakaosimama ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Bashungwa ameyasema hayo leo Disemba 20, 2022 katika hafla ya mapokezi yake wakati alipowasili mkoani Kagera ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipochanguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kauli mbiu ya Kazi iendelee amehakikisha Miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano inaenendelea kutekelezwa na hakuna mradi uliosimama” amesema Bashungwa

Bashungwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa ya kupeleka fedha nyingi za maendeleo kote nchini kuanzia ngazi ya kijiji mpaka miradi ya kitaifa kama Ujenzi wa reli ya SGR na bwawa la kuzalisha umeme la Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambayo yote inaendelea kutekelezwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!