Home Kitaifa UZINDUZI WA CHAMA CHA WAMILIKI MATIPA NA MITAMBO KIZINDULIWA NA NAIBU WAZIRI...

UZINDUZI WA CHAMA CHA WAMILIKI MATIPA NA MITAMBO KIZINDULIWA NA NAIBU WAZIRI ATUPELE

Na Magreth Mbinga

Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete (Mb) anatarijiwa kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa chama Cha wamiliki wa Matipa na Mitambo Tanzania ( TTMOA) Novemba 25 mwaka huu katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama Cha TTMOA, Emmanuel Moshi amesema kuwa katika uzinduzi huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo maafisa waandamizi wa Serikali, vyama vya Sekta binafsi, Jumuiya ya wafanyabiashara na washirika maendeleo.

Aidha, amewataka wamiliki wa Matipa na Mitambo kujiunga Chama Ili kufanya kazi kwa pamoja kukuza uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa watanzania, na kuongeza kuwa licha ya uchanga ulichokuwa nacho chama hicho lakini kimeendelea kukua na kwa sasa ina jumla ya wanachama zaidi ya 150 na ikifanya kazi ndani ya malengo yake.

Hata hivyo, amesema lengo kuanzishwa kwa chama hicho ni kuunganisha, kuwakilisha na kutetea maslahi ya Jumuiya ya wamiliki wa matipa na mitambo nchini Tanzania, ambapo hiyo ni kupitia Sera, utetezi na ushawishi wanapofanya kazi na Serikali kwa niaba ya wanachama wao.

Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya GF Trucks na Equipment, Smart Deus amesema kuwa kampuni hiyo iliamua kudhamini Chama hicho Ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha watanzania kupata ajira.

Tumeona kuwa wengi wa wateja wetu ni wanachama wa chama hichi kwa hiyo ikatusukuma kudhamini chama hichi kwa lengo la kukuza ajira, pili wateja wetu na kuhamisisha na kuunga mkono juhudi za Viwanda Tanzania

Aidha, amesema kuwa, wanachama wao kuwepo katika chama hicho kinawarahisishia wao wanapokuwa na bidhaa mpya kuweza kuwafikia wateja wao kwa haraka kwani wamekua na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wateja wao wanaponunua bidhaa zao ikiwemo magari na mashine hivyo umoja huo umewasaidia sana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!