Home Kitaifa UWT YAFANYA KONGAMANO KUMPONGEZA RAIS SAMIA MAPINDUZI SEKTA YA AFYA.

UWT YAFANYA KONGAMANO KUMPONGEZA RAIS SAMIA MAPINDUZI SEKTA YA AFYA.

Na Boniface Gideon, TANGA

Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga,leo imefanya kongamano maalumu la kumpongeza Rais Samia kwakufanya Mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya hali iliyopelekea kupata tuzo ya kimataifa.

kongamano hilo limefanyika katika viwanja vya Urithi jijini Tanga, ambapo Waziri wa Afya Jenista Mhagama alisema,Wizara ya Afya nchini imepiga hatua kubwa hususani katika huduma za Mama na mtoto ambapo vifo vitokanavyo na uzazi vimeshuka kwakiwango kikubwa,
“tunapozungumzia huduma za Mama na mtoto,tunamaanisha Mama kujifungua Salama bila mmojawapo Kati ya Mama au mtoto kutokupoteza maisha,tumepiga hatua kubwa sana kiukweli,kwasasa hatuzungumzii mama kupoteza maisha wakati wa kujifungua”Aliongeza Mhagama

Mhagama alisema kuwa, katika sekta ya Afya nchini imeendelea kupiga hatua kubwa ambapo zaidi ya wagonjwa 5000 kutoka mataifa jirani walikuja kupata matibabu ya kibingwa,
“Kwa mwaka 2024 , zaidi ya wagonjwa 5000 kutoka mataifa jirani walikuja kupata matibabu nchini,hii ni hatua kubwa sana kwa Taifa letu,tutaendelea na tunajivunia hilo, tutaendelea kuongeza ufanisi katika sekta ya Afya ili kutoa huduma Bora za Afya kwa Wananchi wetu”Aliongeza Mhagama

Kuhusu ukarabati wa majengo ya Hospitali ya Rufani Mkoa wa Tanga ‘Bombo’, Kairuki alisema, Wizara hiyo ipo kwenye hatua za Mwisho nakwamba hivi karibuni ukarabati wa majengo ya Hospitali hiyo utaanza,
“Kule kwenye wodi ya akinamama pale Bombo na majengo mengine,tutaanza kuyakarabati hivi karibuni,tunataka Wananchi wetu wapate huduma nzuri zaidi za Afya , kwahiyo wakazi wa Tanga msiwe na Wasiwasi juu ya Hospitali yenu,lakini pia tunaenda kujenga vituo vingi zaidi vya Afya ,lengo ni kuhakikisha mwananchi hatembei zaidi ya km 5 kwenda kutafuta huduma za Afya”Aliongeza Mhagama

     Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!