Home Kitaifa UWT NA APS WAGAWA TAULO ZA KIKE

UWT NA APS WAGAWA TAULO ZA KIKE

Na Mwandishi wetu, Mzawa Online

Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Kata ya kunduchi kwa kushirikiana na Kampuni ya APS leo wametoa msaada wa Taulo za kike kwa wanafunzi wa kike shule ya Mtakuja Beach Sekondari 8/8/2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti UWT Kata ya Kunduchi Twilumba Jane Balama wakati akikabidhi taulo hizo amesema kuwa lengo ni kusapiti elimu kwa wanafunzi wa kike waweze kuendelea na masomo yao.

“Leo tumeshirikiana na kampuni ya APS kuja kugawa taulo za kike, nimeambatana na viongozi wa chama wakiwemo Katibu wa UWT Kunduchi Moshi kinyage pamoja na mjumbe wa Halmashauri kuu UWT Hellen Mwang’onda pamoja na mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Happy Mhango, hii ni katika utekelezaji wa ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM”amesema Twillumba.

Aidha, amesema huo hautokua mwisho wamejipanga kuwafikia wanafunzi wengi zaidi, huku akiwataka wanafunzi hao kuweza kujikubali na kujithamini na kuhakikisha wanakua wasafi muda wote, ikiwa lengo la kugawa taulo hizo ni kuhakikisha wanafunzi hawakosi masomo yao kwa kukosa taulo hizo.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtakuja Beach Janeth ameishukuru UWT kwa kushirikiana na Kampuni ya APS kwa kufika shuleni hapo na kutoa misaada ya taulo hizo kwani uhitaji bado ni mkubwa kwa wanafunzi hivyo amewataka na wadau wengine kuweza kujitokeza kusaidia kutoa taulo za kike.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!