Home Kitaifa UWEKEZAJI WA NYIHITA BUTIAMA WAMFURAHISHA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE

UWEKEZAJI WA NYIHITA BUTIAMA WAMFURAHISHA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE

Na Shomari Binda-Butiama

KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amefurahishwa na kupongeza uwekezaji uliofanywa na mfanyabiashara mzawa Wilfredy Nyihita wilayani Butiama

Pongezi hizo amezitoa leo agosti 1/2024 mwenge wa uhuru ulipotembelea na kufungua nyumba ya huduma za kulala,vyakula na vinywaji ya Nabaki Africa Motel hiyo iliyojengwa na mfanyabiashara huyo iliyopo Kijiji cha Nyabange Kata ya Nyankanga.

Amesema wamepokea taarifa ya mradi huo na kuupitia kisha kujilidhisha na kuamua kuufungua ili kusaidiana na serikali kutoa huduma kwa watanzania na wageni kutoka nje.

Mnzava amesema amesema serikali inatambua mchango wa sekta binafsi na ipo tayari kuwapa ushirikiano pale unapo hitajika.

Amesema taarifa imeeleza namna mradi huo utakavyowezesha ajira kwa watanzani watakafanya kazi kwenye Motel hiyo.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge amesema wanapongeza sana mradi huo na kuamua kumkabidhi kuushika mwenge mfanyabiashara na muwekezaji huyo na kutoa wito kwa mkuu wa wilaya kuulinda na kumpa ushirikiano.

” Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anataka sekta binafsi ipewe ushirikiano kwenye shughuli zao ili kulinda mitaji yao kwenye miradi wanayo wekeza.

” Nyihita amefanya kazi nzuri na kubwa niendelee kumpongeza sana na tumpe ushirikiano kwenye miradi yake ili awasaidie watanzania wenzake kwenye suala la ajira”,amesema.

Akisoma risala kwa kiongozi wa mbio za mwenge mkurugenzi wa Nabaki Africa Motel Nyihita Wilfred Nyihita amesema kwa kuanza mradi huo umetoa ajira 16 na nyingine zitaongezeka kutokana na uhitaji.

Amesema moja ya lengo la mradi ni kuongeza ajira na kupambana na vitendo vya uhalifu kwenya jamii na kuomba kupewa ushirikiano.

Nyihita ameishukiru serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mazingira wezeshi kwa wawekezaji wazawa kupitia sera ya uwezeshaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!