Home Kitaifa UWEKAJI SERA,SHERIA NA MIFUMO MADHUBUTI KATIKA UPATIKANAJI WA NISHATI SAFI NA SALAMA

UWEKAJI SERA,SHERIA NA MIFUMO MADHUBUTI KATIKA UPATIKANAJI WA NISHATI SAFI NA SALAMA

Waziri wa nishati JANUARY MAKAMBA amewataka watanzania kutoweka vikwazo katika kutafuta njia pekee ya kuondokana na nishati chafu badala yake watafute njia pekee nini kifanyike ili kuraisisha upatikanaji wa nishati safi na salama kwa Taifa zima .

Hayo yamesemwa leo Novemba 2,2022, wakati akiendelea kuongoza mjadala wa siku ya pili wa nishati safi ya kupikia unaendelea katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Aidha Makamba amesema ili kupata mafanikio kwa taifa zima ya upatikanaji wa Nishati safi na Salama serikali itahakikisha Sera ,sheria na mifumo madhubuti inawekwa vizuri huku akiwataka wadau ambao wanafikiri kuanzisha nishati safi mbadala kujitokeza kwani atashirikiana nao katika kutatua changamoto hiyo.

Ili tupate mafanikio upatikanaji wa Nishati safi ni lazima kuwe na Sera na Sheria iwekwe vizuri“. Amesema Makamba.

Naye Mkuu wa mkoa wa Iringa HALIMA DENDEGO amesema upatikanaji wa nishati safi kwa watanzania inawezekana kutokana na uwepo wa vyanzo vingi vya uzalishaji pamoja na kuongeza utoaji wa elimu kwa jamii nzima huku akiahidi kuweka kipaumbele katika kuhamasisha wananchi mkoani humo kupata nishati safi ya kupikia.

Watanzania kupata Nishati safi na salama inawezekana kutokana na vyanzo vingi vya uzalishaji,pia elimu itolewe Kwa jamii nzima kuhusu kutumia nishati safi ya kupikia“. Amesema Dendego.

Kwa upande wake Mhadhili kutoka katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro Profesa ROMANUS ISHENGOMA ameishauri serikali kupitia Wizara ya Nishati lazima ijumuishe matumizi ya vyanzo mbadala ambavyo vinapatikana katika mazingira yanayowazunguka Wananchi, kwani Mitungi ya Gas ya LPG inatoka kutoka nje ya Nchi

Lazima tuweke sera za kipindi cha mpito ili kuepuka utegemezi wa nishati mbadala ambayo inatoka nje ya Nchi, bali tutumie vyanzo halisi ambavyo vinapatikana katika mazingira yetu ambavyo tutaweza kupata Nishati Safi na endelevu, mfano Umeme wa maji, jua na Biogas“. amesema Ishengoma.

Naye mkurugenzi mkuu wa Taifa Gas HAMIS RAMADHAN amesema kamati itakayotengenezwa kuunda Sera na sheria pamoja na mifumo ya uwezeshaji wa upatikanaji wa nishati hiyo iweke mkakati mzuri kumuwezesha kila mtanzania kupata nishati hiyo.

Hata hivyo mjadala huu wa kitaifa unamalizika Leo ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwa lengo ni kuweka Sera ,sheria na mifumo mizuri itakayowezesh upatikanaji wa nishati safi kwa Taifa Zima

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!