Home Kitaifa UWEKAJI NGUZO ZA ZEGE MKONDO WA MTO RUFIJI WASAIDIA KUZUIA ATHARI KUBWA...

UWEKAJI NGUZO ZA ZEGE MKONDO WA MTO RUFIJI WASAIDIA KUZUIA ATHARI KUBWA ZA MAFURIKO KATIKA MIUNDOMBINU YA TANESCO

Licha ya mvua kubwa mwaka huu zilizosababisha mafuriko katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Shirika la umeme Tanzania TANESCO limesema ubadilishaji wa nguzo kwa kuweka nguzo za zege zimesaidia kuzuia athari kubwa za mafuriko katika shirika hilo ukilinganisha na mafuriko ya mwaka 2020 ambapo nguzo 60 zilikatikaWananchi walikosa huduma lakini mwaka huu hakuna nguzo zilizoanguka.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Meneja wa TANESCO wilayani Rufiji SAID MASUDI amesema mwaka 2020 katika daraja la Mkapa nguzo 60 zilikatika lakini mafuriko ya mwaka huu hakuna nguzo iliyokatika na hakukuwa na athari zozote zilizosababishwa na mafuriko hayo kwenye miundombinu ya umeme.

Ubadilishwaji wa nguzo za miti unaoendana sambamba na uwekaji wa nguzo za zege umesaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na athari za kimazingira ikiwemo mafuriko na hii inaashiria kuwa nia ya serikali ya kumtoa mwananchi wake gizani inakwenda kutimia.

Amesema katika wilaya hizo za Kibiti na Rufiji mafuriko hayo hazijaathiri miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo za zege na hii inatoa ishara kwamba shirika limedhamiria kwa dhati kutokomeza tatizo la kukatika katika kwa umeme nchini.

MASUDI amesema kipindi kabla ya mvua kubwa walifanya matengenezo makubwa ikiwemo kubadilika nguzo za miti na kuweka nguzo za zege sehemu kubwa sana hasa katika eneo ambalo maji ya mto Rufiji yanakatisha.

Ameyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Barabara ya kwenda Mloka huko Kipo, Ngalambe, Mbambe, Mpima, na maeneo yote yaliyokuwa ni mkondo wa maji kumeimarishwa kwa kumewekwa nguzo za Zege na ndio maana tumekuwa imara katika hiyo miundombinu.

Hata hivyo amesema Shirika hilo limejihimarisha katika uwesambazaji wa umeme wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vifaa vya uwekezaji wa umeme majumbani hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupeleka maombi yao ili wawekewe umeme.
+++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!