Wazo la Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda tunalo mwaka wa nne sasa tumelipokea vizuri linalengo la kusaidia waandishi na wasomaji wa riwaya endapo Serikali itatoa fungu la kusaidia kuchapiaha vitabu na kupeleka sokini.
Hayo yamezungumzwa na Katibu mwenezi wa umoja wa waandishi wa riwaya wenye dira (UWARIDI ) Maundu Mwingizi na kukanusha kauli ambayo watu wanasema Watanzania sio wasomaji wa vitabu sababu wasomaji wao wengi ni Watanzania.
Pia amesema usomaji umepungua kidogo kwasababu ya kuenea kwa teknolojia ambapo watu wengi wameacha kusoma vitabu wapo zaidi mtandaoni.
“Katika matamasha ya uzinduzi wa vitabu huwa tunashirikisha waandishi hata ambao hawapo uwaridi na msimu huu tulifanya tamasha kubwa na waandishi ambao hawakuwa uwaridi walizindua vitabu vyao kati yao mmoja alipata ngao ya mtunzi “ amesema Maundu.
Sanjari na hayo amundu amesema endapo watashikwa mkono na wadau mbalimbali watafanya matamasha mengi zaidi sababu tamasha lililopita waliongeza vitu vingi ambavyo vinavutia vijana ambavyo vinapatinkana katika katamasha mengine.