Home Kitaifa UVCCM yapongeza serikali kuimarisha sekta ya Uwekezaji

UVCCM yapongeza serikali kuimarisha sekta ya Uwekezaji

Na Neema Kandoro , Mwanza

UMOJA wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana umepongeza kwa kauli moja juhudi zinazofanywa na serikali kwenye sekta ya uwezeshaji kwani inaharakisha maendeleo hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Mwanza hivi karibuni kwa kauli moja kwenye Kongamano la Umoja wa Vijana (UVCCM) ambapo walijadili kwa kina juu ya masuala ya uwekezaji na sheria zake.

Katibu wa UVCCM Wilayani Nyamagana Ramadhan Omary akisoma taarifa hiyo alisema kuwa wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuitafsiri kwa vitendo ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kwa mapana kuimarisha ustawi wa watanzania wote.

Walisema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa meli kubwa MV Mwanza yenye urefu wa mita 92 yenye uwezo wa kubeba tani 400 za mizigo abiria 1200 kuwa ni miongoni mwa vitu vyenye faida hapa nchini.

Aliongeza kusema kuwa vilevile wamefurahishwa na ujenzi wa daraja kubwa la Kigongo Busisi linalounganisha wilaya ya Misungwi na Sengerema kuwa ni mafanikio mazuri ya kupigiwa mfano.

“Tunaiunga mkono serikali yetu juu ya uamuzi wake wa uwekezaji na uendeshaji wa bandari kwani ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi yetu” ilisema taarifa hiyo.

Walisema miundombnu hiyo ni kichocheo kikubwa kwenye sekta ya usafirishaji hivyo uamuzi uliochukuliwa kwa sasa juu ya uendeshaji wa bandari ya Dar es saam na Kampuni ya DP World kuwa utaleta maendeleo hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!