Home Kitaifa UVCCM WAKABIDHI VIFAA VYA KUSAFISHIA DAMPO LA RWAMISHENYE WATOA NENO KWA MANISPAA...

UVCCM WAKABIDHI VIFAA VYA KUSAFISHIA DAMPO LA RWAMISHENYE WATOA NENO KWA MANISPAA YA BUKOBA.

Na Theophilida Felician Kagera.

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba Mkoni Kagera kwa pamoja wameungana na kujitolea vifaa vya kufanyia usafi dampo la kukusanyia kata lililopo Mtaa wa NHC katani humo.

Vijana hao chini ya katimu wao Imani Sudi Hussein wamechanga changa nakufanikiwa kupata vifaa hivyo ambavyo wamevikabidhi kwa mtendaji wakata Issack .S. Mzinga ili kuwapatia vijana wanaojitolea kukusanya taka za ndampo hilo.

Katibu Imani akizungumzia hilo kwaniaba ya vijana wenzake amesema kuwa kilichowasukuma kufanya hivyo nikutokana na kuwepo kwa kero ya kujaa kwa taka eneo la dampo hilo ambalo lipo karibu na makazi ya wananchi, shule ya msingi Rwemishasha, Machinjio ya wanyama ya Manispaa ya Bukoba pia nakituo cha kufundishia elimu ya awali kwa watoto wadogo.

Katibu huyo amefafanua kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kero ya kujaa uchafu eneo hilo kumekuwepo na baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakijitolea kuzikusanya pamoja taka bila ya vifaa maalumu vyakujikinga usalama wao kiafya jambo ambalo limewasukuma wao kama UVCCM kujimudu na kuwiwa kubuni wazo hilo ambalo pia walilishirikisha Mhe Mbunge na Diwani wakata hiyo.

Tumefanya hivi ili kuunga juhudi za vijana hawa ambao wamekuwa wakizikusanya pamoja taka ili kuepusha kuzagaa zagaa kila mahali tukizingatia dampo hili ni lawazi kiukweli wamekuwa wakifanya kazi kubwa tena bila kulipwa chochote tumeona ni bora tuwawezeshe vifaa hivi japo wafanye kazi hii kwa usalama wa afya zao” ameleeza Katibu Imani Sudi.

Amevitaja vifa hivyo ni pamoja na Grovis, Boots, Ovarory, na Koleo.

Ameendelea kusema kwamba vifa hivyo vitawasaidia vijana hao watatu kutambuliwa vyema wawapo katika kazi yao hiyo ya kusafisha dampo kwani wamekuwa wakizipitia changamoto kadha wa kadha ikiwemo ya kuitwa wezi kutoka na hali yao ya ukusanyaji taka ambazo baadhi yake huzitumia kama ajira kwao baada ya kuziokota nakuziuza hususani chupa za plastik vyuma chakavu nanyinginezo, hivyo ametoa wito kwa uongozi wa kata na mtaa kuwatambua vyema bila ya kuwabughudhi kama ilivyokuwa mwanzo kwani wanasaidia pakubwa kusafisha eneo hilo chafu.

Pia ameiomba Manispaa ya Bukoba kupitia idara ya Mazingira kuhakikisha wanaongeza jitihada za kuzizoa taka kwa wakati kwenye madampo ya mji wa Bukoba kwani wananchi wamekuwa wakilipa tozo za taka hivyo nimuhimu sana mazingira yao kuwa safi na salama bila ya taka kuzagaa zagaa kila kona huku akiongeza kuwa kinapokuwa kimeibuliwa kikundi cha vijana wenye uwezo wa kufanya usafi wa mazingira maeneo mbalimbali kipatiwe usajili ili kuongeza ufanisi zaidi wakuusafisha mji wa Bukoba ikiwemo kata ya Rwamishenye.

Hata hivyo amewasihi wananchi wa eneo lilipo dampo hilo kuendelea kuwa wavumilivu wakati juhudi za Serikali zikiendelea ili kuweza kupata ufumbuzi sahihi wa adha ya taka za eneo hilo.

Aidha ametoa shukrani zake kwa vingozi wanaondelea kuwa nao bega kwa bega katika kuyatekeleza majukumu kadha wakadha ya kimaendeleo yote hiyo ikiwa nikuunga kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yakuwaletea maendeleo wananchi hapa nchini bila kumsahau Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Diwani na watendaji wakata wenyeviti wa mitaa na wajumbe, sambamba na vijana wenzake ambao ameambatana nao katika kutekeleza zoezi hilio.

Diwani wakata hiyo Mhe Suwedi Juma Kagasheki amesema kwamba kero ya dampo hilo niya muda mrefu japo amekuwa akifanya juhudi za kila namna kwa mkutadha wakuitatua changamoto hiyo kwa wananchi ambapo tayari suala hilo amelifikisha kwa Afisa mazingira wa Manispaa ya Bukoba.

Tumekaa nauongozi wa baraza la madiwani kuona ni sehemu ipi kuweza kuweka ndapo lakini kila mwaka unapokwenda wanasema bajeti Mkurugenzi anasema bajeti bajeti mimi nakamati ya maendeleo ya kata kila siku napokuwa nahoji hiki kitu Afisa mazingira anasema ameweka kwenye bajeti lakini mimi sitasita kumkumbushia kila siku ni kwanini dampo linakuwa wazi namna hii likikaa wazi hivi ni hatarishi wanafunzi wanapita na watu wengine wanapita mvua ikinyesha hali ya hapa si shwari vijana wa UVCCM nawahidi ntaendelea kulipambania” Amewaeleza vijana hao Diwani Suedi Juma.

Amewapongeza vijana kwakufanya jambo hilo zuri kwani ni watu wamfano na wakuigwa wakiendelea hivyo watayafanya yaliyo makubwa na mazuri mno kwenye jamii.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Bi Shani Kombo wamewashukuru nakuwapongeza vijana hao pamoja na viongozi wengine kwakutekeleza tukio hilo muhimu ambalo litasaidia kupunguza adha ya uchafu wanao kumbana nao eneo hilo maana nyakati za mvua harufu mbaya huwa kali zaidi huku wakiahidi kuendelea kuwa nao vijana hao kwakila jambo liwe lakimaendeleo amala laa!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!