Home Kitaifa UVCCM UBUNGO YAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA DC. MPYA

UVCCM UBUNGO YAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA DC. MPYA

Baraza la Vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) limempongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake nani kuendelea kuwa mfano na mwenye kuleta matumaini makubwa kwa watanzania.

hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ubungo Shadrack Makangula wakati akiongoza kikao Cha Baraza la Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ubungo

Aidha Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya aliweza kumkaribisha Mkuu wilaya ya Ubungo Mhe. HASSAN BOMBOKO kwenye BARAZA hilo na kumueleza kuwa watu wa Ubungo wanajiona wenye bahati kwa kuwa wanapata bahati mara kwa mara ya kuongozwa na wakuu wa wilaya vijana na kuahidi kumpa ushirikiano.

Pamoja na mambo mengine DC Bomboko aliwashukuru vijana wa Ubungo kwa namna walivyompokea na kuahidi kutoa ushirikiano wake Mkubwa. Pia ameahidi kuleta Makongamano, Semina na maswala ya fursa za kiuchumi na kuwapa Ushirikiano wakutosha Ili kufanikisha hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!