Home Kitaifa UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAMUUNGA MKONO RAIS DKT SAMIA SULUHU...

UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAMUUNGA MKONO RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Pichani katikati anayezungumza ni Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam Nasra Mohammed

Na Magrethy Katengu

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam umewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono kwa kuonyesha umahiri wake na uwezo wa kuwaongoza na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salam Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohamed akizungumza wakati akitoa tamko juu ya mjadala kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii wa uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai pia amewataka wanasiasa kuacha kutumia vibaya Demokrasia waliyopewa na Rais Dkt. Samia kwa kuvuruga amani na utulivu na kusababisha taharuki kwa kutoa kauli ambazo ni hatari .

Nasra amesema uamuzi alioufanya Rais Dkt. Samia umewagusa vijana hao kwa kuzidi kuonesha ni kiongozi msikivu kwani kipindi cha nyuma palikuwa na malalamiko kwa nini serikali haipeleki mikataba inayohusisha uwekezaji mkubwa wenye maslahi mapana ya nchi bungeni ijadiliwe kwa uwazi kila mwananchi asikie na atoe maoni yake .

Hii imedhihirisha ukomavu wa uongozi, umahiri na umakini wa Rais Dkt. Samia, tunampongeza kwa anavyoendelea kutafsiri kwa vitendo kuonesha uwazo bila kificho ambapo kwa eneo la utawala bora, utawala wa sheria na madaraka kwa wananchi imewekwa wazi kwami huko nyuma mikataba ilikuwa ikisainiwa bila kujadiliwa na kutolewa maomib,” amesema Nasra.

Hata hivyo Nasra amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameonesha kwa dhati kwa kauli na vitendo kuwa yeye ni mwanademokrasia makini kwa kuwa na uongozi mahiri anayewasikiliza wananchi wake akithibitisha kwa kusema na kutenda.

Rais Dkt. Samia ameendelea kusisitiza kuwa yupo tayari kupokea na kusikiliza maoni mbalimbali, kushauriwa na kukosolewa kwa hoja sio matusi , hivyo tunawataka wanasiasa waliofilisika hoja wasitumie udemokrasia wa Rais Dkt. Samia vibaya kuvuruga amani na utulivu na kusababisha taharuki kwa kutoa kauli ambazo ni hatarishi nchini,” amesisitiza Nasra.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!