Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro akiwa pamoja na wataalamu wa ardhi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri Ikungi leo tarehe 27/07/2022 wamesikiliza na kumaliza kero ya mgogoro wa viwanja vya wananchi 40 katika kijiji Muungano kitongoji samumba
Awali mgogoro huo ulishasikilizwa na kutolewa maamuzi na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Edward Mpogolo ambae kwa sasa ni Mkuu wa wklya ya ambapo hata hivyo baada ya kuhamishwa utekelezaji wa maamuzi yake ulikumbwa na changamoto ambayo Dc Muro ameimaliza kwa kuelekeza maamuzi ya awali yasimamiwe na kutekelezwa ipasavyo ndani ya siku 30 kuanzia leo
Dc Muro amefikia uamuzi huo baada ya kuwasikiliza wananchi hao pamoja na vielelezo vyao na kusikiliza upande wa pili wa familia ya Marehemu Mujungu ambao walivamia maeneo hayo na kuuza viwanja kwa watu wengine wakati wakijua hawakuwa na haki ya kufanya hivyo hatua iliyozua mgogoro kutoka kwa wananchi wa awali waliopewa viwanja hivyo na uongozi wa kijiji cha Muungano tangu mwaka 2016
Dc Muro amewaelekeza maafisa ardhi wa halmashauri kuendelea na mchakato wa kupima viwanja katika eneo hilo ili wananchi 40 waweza kupewa haki yako na kumtaka afisa ardhi kutoa notisi ya siku 30 kwa watu waliovamia eneo hilo kwa kununua viwanja kwa mtoto wa Marehemu Mujungu ambae ametakiwa kuwarudishia wananchi hela alizochukua
Awali mgogoro huo ulishasikilizwa katika baraza la ardhi la kata na maamuzi na serikali ya kijiji kushinda jambo ambalo lilisababisha familia ya mujungu kwenda kukata rufaa baraza la ardhi la wilaya ambapo maamuzi ya baraza yalirejesha jambo hilo tena baraza la ardhi la kata lisikilize tena kutoka na dosari zilizojitokeza hapo awali hatua ambayo iliwalazimu familia ya mujungu kukaa meza moja na uongozi wa serikali ya kijiji cha muungano na kulimaliza jambo hilo kwa kuandikishiana muafaka ambao familia iliridhia na kusaini kwa kupatiwa viwanja viwili katika eneo hilo uku eneo lingine kubwa likirejeshwa katika serikali ya kijiji
Pamoja na kuwepo kwa nyaraka za muafaka huo familia ya mujungu ilipinga nyaraka walizosaini wenyewe na kuibua upya mgogoro huo ambao leo Dc Muro amehitimisha kwa kuelekeza makubaliano ya awali yaheshimiwe na watu wafuate utaratibu na makubaliano waliyowekeana.