Na Mwandishi Wetu.
Usiku wa Machi , 06 , 2024 Tuzo za heshima kwa viwango vya Ubora wa bidhaa na huduma kutoka Superbrand East Africa Choice 2022/2024 zimetolewa kwa Kampuni na Mashirika mbalimbali yanayojihusisha na Uuzaji, Ununuzi na utoaji wa huduma mbalimbali kwa Umma, Tuzo zilizofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Ikumbukwe ,Tuzo hizi hutolewa na baraza la superbrand kutoka Afrika Mashariki kufuatia mchakato yakinifu uliohusisha kampuni mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kila mwaka maelfu ya bidhaa kutoka sekta tofauti zinaamuliwa dhidi ya vigezo vitatu vya muhimu vya Superbrand: ubora, kuaminika na utofauti. Kufikia hali ya kutunukiwa hadhi ya Superbrands ina maana hadhi ya bidhaa husika inaongezeka na huwahakikishia watumiaji na wauzaji kuwa wananunua bidhaa iliyobora kabisa.
Akizungumza na Mwandishi Wetu , Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ambao ni miongoni mwa Makampuni yaliyoshinda Tuzo hiyo , Abdallah Asas amewashukuru waandaaji wa Tuzo hizi kwa kuongoza mchakato vyema wa uandaaji na utoaji wa Tuzo hizi,
‘Kipekee nichukue nafasi hii kuwashukuru waandaji wa tuzo hizi za Superbrand, kushinda tuzo hii ni ishara tosha ya juhudi za Uzalishaji, Usambazaji na uuzaji wa Maziwa yetu nchini kuendelea kuwa bidhaa muhimu katika jamii’- Abdallah Asas Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa Maziwa
Hizi ni baadhi ya picha mbalimbali za tukio la utoaji wa Tuzo hizo lililofanyika Jijini Dar Es Salaam Usiku wa Machi 6