Home Kitaifa USAMBAZAJI MAJI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI KUANZA MWEZI UJAO

USAMBAZAJI MAJI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI KUANZA MWEZI UJAO

Na Shomari Binda-Musoma

MIRADI ya usambazaji maji kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Musoma vijijini inatarajiwa kuendelea mapema mwezi ujao.

Miradi itaendelea kwenye maeneo hayo kutokana na kupatikana kwa wakandarasi watakaotekeleza miradi hiyo.

Katika vijiji 68 ndani ya jimbo hilo ipo miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa na maeneo mengine tayari wananchi wameshapata maji.

Usambazaji wa maji kutoka kisima kirefu cha Kijiji cha Kinyang’erere mkandarasi wa kusambaza maji kutoka kisima cha kina kirefu kilichochimbwa Kijiji cha Kinyang’erere amepatikana na kazi anaanza mwezi ujao.

Tenki na mabomba kwa Kata za Busambara na Kiriba mkandarasi amepatikana kuanza kujenga miundombinu ya kusambaza maji kwenye Kata za Busambara na Kiriba na ataanza kazi mwezi ujao.

Mkandarasi atajenga Tenki lenye ujazo wa Lita 500,000 (laki 5) kwenye mlima wa Mwiringo.

Maji kutoka kwenye Tenki hilo ndiyo yatasambazwa ndani ya Kata za Busambara na Kiriba.

Wananchi wameombwa watoe ushirikiano mzuri kwa wakandarasi wawili wakiwa kwenye maeneo ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!